Oct 13, 2015
Mambo 10 Unayotakiwa Kuyaacha katika Maisha Yako.
Siku
zote maisha ya mwanadamu yanaaongozwa na miiko
au kanuni. Ni miiko hiyohiyo ambayo ilianza toka zamani lakini ambayo lengo
lake kubwa lilikuwa ni kutuelekeza mambo yapi tufanye na mambo yapi tusiyafanye
katika maisha ili tufanikiwe. Wale waliofuta miiko hiyo ni kweli walifanikiwa, na wale walioikiuka walishindwa
katika maisha yao kwa naman fulani.
Kwa
bahati mbaya au nzuri miiko au kanuni
hizo zinafanya kazi katika maisha yetu mpaka sasa. Wengi huwa hawajui katika
hili, lakini upo umuhimu mkubwa sana wa kuijua na kuifuata hiyo miiko au kanuni na kuamua kuachana na
mambo ambayo yanawezayakawa kizuizi kwetu cha mafanikio. Katika makala hii
tutaangalia mambo ambayo ni lazima tuyaache ili tufanikiwe.
Yafuatayo Ni Mambo
Unayotakiwa Kuyaacha katika Maisha Yako.
1.
Acha kuruhusu makosa madogo madogo, hatimaye yakawa makosa makubwa na
yakakuzuia kufanikiwa .
2.
Acha kukimbia changamoto zinazokukabili, pambana nazo mpaka ufanikiwe na
kufikia mafanikio makubwa katika maisha yako.
3.
Acha kusahau kule ulikotokea. Yapo mambo ya kujifunza kutokana na kule
tulikotoka.
4.
Acha siku zote kujijengea tabia ya kulalamika. Kama utaebndelea kufanya hivyo
utashindwa katika mambo yako mengi sana .
5.
Acha kamini kuwa utashindwa kwa kile unachokifanya. Kila mara na kila wakati
amini wewe ni mshindi wa maisha yako.
6.
Acha kuruhusu pesa ikakutawala. Matokeo yake itawale pesa na hiyo itakusaidia
kufikia uhuru wa kipesa.
7.
Acha Kurusu hofu ikakutawala maisha yako. Kwa kadri utakavyozidi kuwa na hofu
ndivyo ambavyo maisha yako yatazidi kuwa mgumu. Hiyo yote ni kwa sababu
utashindwa kufanya mambo yako kwa sababu ya hofu ulizonazo.
8.
Acha kuanzisha biashara, huku ukiwa unategemea bahati ndiyo ufanikie. Ondoa
mawazo ya bahati na fanya biashara yako kwa kujimini, utafanikiwa.
9.
Acha kujijengea tabia ya kufurahia, hasa ple mambo yaw engine yaopkuwa mabaya.
Badala yake wape moyo na kuwafariji.
10.
Acha kuogopa kusonga mbele, hata kama kuna wakati unahisi kama vile unakwama.
Wewe endelea kukazana na kusonga mbele na mwisho wa siku utafanikiwa.
Yapo
mambo mengi sana yanyokulazima kuacha maisha yako ili kufanikiwa na kuishi
maisha amani. Kwa leo jifunze kitu kupitia mambo hayo na maisha yako yatakuwa
yatofauti.
Nakutakia
kila la kheri katika safari yako ya kuboresha maisha yako na endelea kutembelea
DIRA YA MAFANIKIO kujifunza na kuhamasika.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani
Ngwangwalu,
Kama una maoni, ushauri au changamoto yoyote inayokuzuia kufikia mafanikio
yako wasiliana nami kwa email dirayamafanikio@gmail.com au simu 0713 048035
kwa ushauri na msaada wa haraka.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.