google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Aug 2, 2021

Hivi Ndivyo Unavyoweza Kutengeneza Historia Ya Maisha Yako.

No comments :

Amua kuandika historia ya maisha yako kwa kuamua kufanya kile unachokipenda na tena kwa nguvu zako zote. Waonyeshe watu kwa vitendo kwa kile unachokifanya hubahatishi, bali unakijua ndani, pia unakijua kwa nje.

Kipi unachokifanya, basi kitu hicho amua kukifanya kwa ubora wa juu na kikupe matokeo makubwa unayoyataka. Hakikisha unachokifanya kinakufanikisha na kinakupa matokeo makubwa ambayo kila mtu atashangaa.

Andika historia kubwa ya maisha yako kwa hicho ukifanyacho. Kifanye mpaka watu wengine watakaotokea nyuma waje washangae ulifanyaje. Kuwa shujaa wa maisha yako mwenyewe kwa kufanya makubwa na ya kutisha.

Kama kuna watu walitengeneza historia ya maisha yao kwa jasho na damu, wewe leo, tengeneza historia ya maisha yako kwa kuamua kuchapa kazi, na kuchapa kazi mpaka kieleweke. Kazi yako ndio itaandika historia mpya ya maisha yako. 

Hakuna kinachoshindikana, inawezekana kutengeneza historia kubwa ya maisha yako kwa kuamua kufanya mambo makubwa. Uamuzi upo kwako, je uko tayari kufanya mageuzi makubwa ya maisha yako. Kama uko tayari, acha kusubiri, anza sasa na bila hofu.

Anza kuchapa kazi, weka juhudi kwa nguvu zote, jitume sana, nakwambia historia kubwa ya maisha yako utaiandika na wengi watashangaa, jinsi ambavyo utakuwa umefanya maisha yako kuwa bora. Kila kitu kinawezekana chini ya jua, kama iliwezekana kwao, hata kwako inawezekana pia.

Kila la kheri katika kufikia mafanikio yako.

Kama unapenda kujiunga na kundi la mafanikio ili uweze kujifunza zaidi mambo mengi ya kimafanikio. Tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER'S kwenda 0687449428 na utapewa utaratibu wa kuunganishwa.

Hakimiliki©2021 Imani Ngwangwalu. Haki Zote Zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha yako. Ruksa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ya ruhusa ya mwandishi.

 

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.