google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Aug 14, 2021

Tumia Nguvu na Uwezo Wako Hivi, Utafanikiwa.

No comments :
Tumia Uwezo Wako Kufanikiwa

Ikiwa gari yako imepata panja, na ukaipeleka gereji, ili kuweza kutoa tairi hiyo na kubadilisha nyingine, ni wazi utatakiwa uchukue jeki inyanyue gari na utoe tairi. Hata kama ungekuwa na nguvu sana, kunyanyua gari kwa mikono usingeweza.

Lakini kwa kutumia jeki, utanyanyua kidogo kidogo tena bila kutumia nguvu nyingi na unashangaa mwisho wa siku gari inanyanyuka na kutoa hilo tairi. Kitu ambacho kimerahisha ni jeki na nguvu ambayo ilikuwa ikitumika ni kidogo sana. 

Turudi kwenye maisha ya kawaida, ikiwa umejiwekea malengo yako, na unataka kuyatimiza kwa siku chache sana,  pia ni jambo ambalo hutaweza kufanikiwa, hata kama una rasimali nyingi na za kutosha kukufanikisha. 

Ikiwa lakini ungekuwa umeweka nguvu zako kidogo kidogo, katika kuyafikia malengo, mwisho wa siku unajikuta umefika kule unakotaka kufika, kwa kuchukua hatua kidogo kidogo tena kila siku.

Ipo wazi una nguvu na uwezo mkubwa wa kufikia mafanikio yako.  Nguvu na uwezo huo hutakiwi kuutumia mara moja, bali ni kidogo kidogo hadi unafanikiwa. Nguvu kubwa ya mara moja, haina uwezo wa kushindana na nguvu inayowekwa kidogo kidogo tena kwa miaka mingi.

Amua leo kuutumia uwezo na nguvu zako kufanikiwa. Chukua hatua kidogo kidogo kila siku, na mwisho wa siku utafanikiwa. Juhudi za kila siku zina matokeo makubwa sana kwako. Kama ulikuwa hulijui hili, nikwambie anza sasa, na utakuwa mshindi.


Kila la kheri katika kufikia mafanikio yako.

Kama unapenda kujiunga na kundi la mafanikio ili uweze kujifunza zaidi mambo mengi ya kimafanikio. Tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER'S kwenda 0687449428 na utapewa utaratibu wa kuunganishwa.

Hakimiliki©2021 Imani Ngwangwalu. Haki Zote Zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha yako. Ruksa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ya ruhusa ya mwandishi.

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.