google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Aug 1, 2021

Kama Utajitengenezea Ujasiri Huu, Tayari Umefanikiwa.

No comments :

Inataka ujasiri kuwa mkarimu, kwa mtu ambae anaonyesha ujeuri wa wazi kwako. Hapa ujasiri na busara zinatakiwa.

Inataka ujasiri kuwa mkweli, kama uongo ndio imekuwa niia rahisi na nyepesi kwako, kwa hapo ujasiri unatakiwa.

Inataka ujasiri kufanya kile unachoendelea kufanya, wakati mazingira hayakuruhusu kufanya yaani sio mazingira rafiki. 

Inataka ujasiri kuendelea kukutana na changamoto, wakati njia ya kukata tamaa tayari inakuwa  inaonekana iko wazi. 

Inataka ujasiri kwa wewe, kufanya yale yaliyo haki, mara kwa mara bila kuyumbishwa na kitu chochote mbele yako.

Inataka ujasiri sana, kwa wewe kukataa vishawishi, ambavyo umewekewa mbele yako. Ujasiri unatakiwa ili kukataa.

Inataka ujasiri pia kwa wewe, kuitengeneza kesho yako. Hapa mengi unatakiwa ujinyime na uvumilivu mkubwa unatakiwa. 

Inataka ujasiri kuendelea kuweka juhudi za kufikia ndoto zako, wakati unaona njia ya kuweka visingizio ni nyepesi kwako.

Na wakati huo huo unatakiwa ujue, ujasiri unakuja kutokana na kufanya yale yaliyo haki. Ujasiri unakuja kutokana na ukweli. Ujasiri unakuja kutokana na unavyoijenga kesho yako. Ujasiri unakuja kutokana na juhudi. Ujasiri pia unakuja kutokana na ung'ang'anizi wako.

Simama imara, kuwa imara, ujasiri wako utakupa unachokitaka. Ujasiri wako utakupa mafanikio. Unao ujasiri tayari. Amua sasa kuutumia ujasiri wako ili ukupe mambo mengi ya mafanikio.

Kama unapenda kujiunga na kundi la mafanikio ili uweze kujifunza zaidi mambo mengi ya kimafanikio. Tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER'S kwenda 0687449428 na utapewa utaratibu wa kuunganishwa.

Hakimiliki©2021 Imani Ngwangwalu. Haki Zote Zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha yako. Ruksa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ya ruhusa ya mwandishi.

 

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.