google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Aug 9, 2021

Ukiweka Juhudi Na Upendo Kwenye Kitu Hiki, Utafanikiwa.

No comments :

Kwa chochote unachokipenda na kukithamini, kifanyie kazi kitu hicho. Weka juhudi kwenye kile unachokipenda na weka upendo kwenye juhudi zako. Kama hakuna juhudi, upendo unakuwa kidogo au hakuna kabisa. Kama hakuna upendo na kujitoa nyuma yake, juhudi zako zote zinakuwa sawa na kazi bure.

Unapokuwa unaipa thamani na kuipenda kazi yako, hakuna kitu cha kuweza kukuzuia kufanikiwa. Kuweka juhudi na upendo kwa kile unachokifanya ni kitu cha muhimu sana ili kufikia mafanikio makubwa.

Elewa katika kila juhudi, kuna changamoto, lakini kwa kuwa ndani yako una upendo wa hicho ukifanyacho, changamoto hizo haziwezi kukuzuia kitu chochote. Kuwa na mtazamo wa kupenda kile unachokifanya, na ukikipenda tu, juhudi lazima utaweka bila kulazimishwa.

KITU CHA KUZINGATIA NA KUELEWA, kila wakati weka juhudi na weka upendo kwa kile unachokifanya, utafanikiwa. Juhudi na upendo wa kufanya kile unachokipenda toka moyoni, huwa vinazalisha mafanikio makubwa wakati wote.

Kila la kheri katika kufikia mafanikio yako.

Kama unapenda kujiunga na kundi la mafanikio ili uweze kujifunza zaidi mambo mengi ya kimafanikio. Tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER'S kwenda 0687449428 na utapewa utaratibu wa kuunganishwa.

Hakimiliki©2021 Imani Ngwangwalu. Haki Zote Zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha yako. Ruksa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ya ruhusa ya mwandishi.


 

 

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.