google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Aug 7, 2021

Ukifanyia Kazi Mambo Haya, Utapata Mafanikio Kila Kona.

No comments :

Ni muhimu sana kuwa na uzingativu na nidhamu katika eneo moja kwanza, ili kupata matokeo makubwa. Kama kila wakati uzingativu na nidhamu utaweka katika eneo moja, basi hilo eneo utafanikiwa sana.

Ipo hivi, unapokuwa na uzingativu na nidhamu katika eneo moja, na ukafanikiwa katika eneo hilo, ni rahisi sana uzingativu huo na nidhamu kwenda katika maeneo mengine, ambayo yanahitaji uzingativu na nidhamu yako.

Kwa mfano, kama umeweka uzingativu na nidhamu ya kupiga zoezi kwa dakika 30 na ukamudu hapo, basi pia uzingativu na nidhamu hiyo unaweza ukaihamisha katika maeneo mengine kama kujifunza na afya.

Unatakiwa ujue, uzingativu na nidhamu, unapofanikiwa katika eneo moja, ni rahisi sana kwenda katika eneo lingine la maisha yako, na ukajikuta kila eneo la maisha yako unalifanya kwa ufanisi mkubwa na mafanikio.

JAMBO LA KUZINGATIA NA KUFANYIA KAZI, kaa ukijua, uzingativu na nidhamu, vinaenea katika maeneo mengine ya maisha yako, kama utafanyia kazi. Hivyo fanyia kazi uzingativu na nidhamu yako, na utafanikiwa.

Kila la kheri katika kufikia mafanikio yako.

Kama unapenda kujiunga na kundi la mafanikio ili uweze kujifunza zaidi mambo mengi ya kimafanikio. Tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER'S kwenda 0687449428 na utapewa utaratibu wa kuunganishwa.

Hakimiliki©2021 Imani Ngwangwalu. Haki Zote Zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha yako. Ruksa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ya ruhusa ya mwandishi.


 

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.