google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Aug 16, 2021

Hizi Ndizo Hatua Ambazo Zinamfanikisha Kila Mtu.

No comments :

Kati ya nguvu kubwa ambayo inaweza ikaleta mafanikio makubwa kwako, ni nguvu ya kuamua kufanya kidogo kidogo. Ukiamua kuchukua hatua kidogo kidogo, hakuna utakachoshindwa kuweza kufanikiwa kwako kwa namna yoyote ile .

Kwa chochote kile ulichoamua kukifanya, nenda kidogo kidogo kama mwendo wa kobe, utashangaa unafanikiwa. Tumia kile ulichonacho na usitake makuu sana kwa mwendo huo mdogo mdogo utafanikiwa na hata usiwe na haraka kubwa.

Ikiwa unafikiria una rasilimali kidogo, hauna maarifa na umekosa fursa fikiria tena kwa upya. Fanya kile unachoweza kufanya. Fanya na kwa kile ulichonacho mkononi, utaweza. Juhudi kidogo kidogo zitakupa mafanikio matokeo makubwa.

Jitahidi ufanye muda uwe rafiki kwako. Fanya kidogo kidogo mpaka utimize ndoto zako. Haina haja ya kukata tamaa, chukua hatua kidogo kidogo kila siku. Weka kazi, na ukiendelea kwa muda mrefu hata kama ni kidogo kidogo utafanikiwa.

Nataka uelewe, ukiamua kutumia utaratibu wa kufanya kidogo kidogo, hakuna kitakachoshindikana. Hata kama huna pesa, ukitumia nguvu hii, utafanikiwa. Hebu Anza kidogo kidogo, hebu chukua hatua kidogo kidogo, utafanikiwa.

Hizi ndizo hatua ambazo zinamfanikisha kila mtu na hata ambae hana uwezo mkubwa. Ipo hivyo kwa sababu ni hatua za kufanya kidogo kidogo, kwa hiyo kila mtu anaweza kuzichukua. Je, bado tu unashindwa kufanikiwa, chukua hatua ndogo, utaweza kufanikiwa.

Kila la kheri katika kufikia mafanikio yako.

Kama unapenda kujiunga na kundi la mafanikio ili uweze kujifunza zaidi mambo mengi ya kimafanikio. Tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER'S kwenda 0687449428 na utapewa utaratibu wa kuunganishwa.

Hakimiliki©2021 Imani Ngwangwalu. Haki Zote Zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha yako. Ruksa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ya ruhusa ya mwandishi.


No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.