google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Aug 30, 2021

Usiwe Mtumwa Wa Jambo Hili, Utakwama.

No comments :


Kuna yale mambo ambayo kwenye maisha huwa yanaonekana ni rahisi kabisa kufanyika na pengine kukupa mafanikio. Hata hivyo kitu cha kushangaza mambo hayo pamoja na urahisi wake wengi huwa hawayafanyi.

Hali hiyo huwa inatokea kwako kwa sababu ya kujikuta upo katika hali ya ‘rahisi kufanya…lakini pia sio rahisi kufanya,’ yaani urahisi kwa hali ya kawaida unauona, lakini ndani yake kuna ugumu fulani hivi ambao unakuzuia kufanikiwa. 

Ukweli wa mambo ulivyo kwenye maisha yako, iwe afya, furaha au utajiri unaweza kuvipata ikiwa utachukua hatua ndogo ndogo kila siku zile zinazowezekana ambazo zitakusogeza kwenye lengo lako bila kudharau hatua yoyote ile.

Kama ni rahisi hivyo, kwa nini watu wengi wanashindwa kufikia malengo yao? Hiyo yote ni kwa sababu ‘rahisi kufanya…lakini pia sio rahisi kufanya,’. Hatua ndogo ndogo zinakuwa ni ngumu sana kuweza kutekelezwa na wengi wetu.

Jiulize ni mambo mangapi katika maisha yako ulipoambiwa fanya kitu hiki, ulisema kwamba, ‘aaah kitu hiki ni rahisi, nitakifanya tu’. Lakini mwisho wa siku unajikuta unashindwa kuchukua hatua kabisa.

Kuanzia sasa, acha kuwa mtumwa wa ‘rahisi kufanya.’ Ukiwa mtumwa wa rahisi kufanya na halafu huchukui hatua utakwama. Hakuna kitu ambacho ni rahisi, kila kitu kichukulie kwa uzito wake mkubwa.

Chukua hatua ndogo ndogo bila kudharau udogo wa hatua hiyo. Kuwa siriaz na maisha yako haswaa. Ukifanya hivyo utaweza kufanikiwa na kutimiza ndoto zako kubwa. Hakuna kinachoshindikana, kila kitu kinawezekana.

Kila la kheri katika kufikia ndoto zako kubwa za kimafanikio.

Kama unapenda kujiunga na kundi la mafanikio ili uweze kujifunza zaidi mambo mengi ya kimafanikio. Tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER'S kwenda 0687449428 na utapewa utaratibu wa kuunganishwa.

Hakimiliki©2021 Imani Ngwangwalu. Haki zote zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha yako. Ruksa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ya ruhusa ya mwandishi.

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.