google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Aug 5, 2021

Mafanikio Hayaendi Kwa Watu Hawa....

No comments :

Mafanikio hayaendi kwa watu wanaosubiri hali au mazingira yawe kamili. Mafanikio yanaenda kwa watu wanaoamua kufanya kwa yale waliyonayo, na kwa wakati wa sasa na sio kusubiri wakati wowote ule.

Mafanikio hayaendi kwa watu wanaosema wako 'bize' na hawana muda, na watafanya kesho au muda mwingine. Mafanikio yanaenda kwa watu wanaojitoa kutafuta muda na kuchukua hatua za kufanya.

Kama wewe ni bado wa kusema huna muda, utafanya kesho, basi nikwambie mafanikio tayari yamekupiga kikumbo cha kwaheri. Mafanikio hayataki watu wa namna hiyo kabisa, yanataka uchukue hatua. 

Unatakiwa ujue mafanikio hayasubiri mtu na hayasubiri hali yoyote iwe nzuri. Ni jukumu lako wewe kutengeneza mazingira yatakayokusaidia katika kufanikiwa kwako na sio mtu mwingine bali ni wewe.

JAMBO LA KUZINGATIA NA KUFANYIA KAZI, elewa mafanikio hayaendi kwa wanaosubiri kesho au kusubiri  mazingira yawe bora. Mafanikio yapo kwa wanaochukua hatua sasa, chukua hatua, utafanikiwa.

Kila la kheri katika kufikia mafanikio yako.

Kama unapenda kujiunga na kundi la mafanikio ili uweze kujifunza zaidi mambo mengi ya kimafanikio.Tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER'S kwenda 0687449428 na utapewa utaratibu wa kuunganishwa.

Hakimiliki©2021 Imani Ngwangwalu.Haki Zote Zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha yako. Ruksa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ya ruhusa ya mwandishi.

 


No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.