Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Monday, January 16, 2017

Chukua Hatua Mapema, Usiruhusu Kufa Na Ndoto Yako.

No comments :
Hebu waza upo hospitalini na umelala kitandani ukiwa hoi kusubiri kifo chako. Kila kitu kuhusu wewe kimeshathibishwa na madaktari kwamba, ni lazima utakufa kutokana na ugojwa unaokusumbua.
Wakati ukiwa kwenye kitanda chako cha kifo, ghafla unakumbuka ndoto na mipango ya aina mbalimbali ambayo ulikiwa hujaikamilisha. Unatamani japo uongezewe muda kidogo ili ukakamilishe mipango hiyo.
Tuchukulie hali hiyo ndiyo imekukuta wewe leo,  je,swali la kujiuliza upo tayari kufa na ndoto zako? Jiulize ni ndoto zipi au kipaji kipi ulichonacho ambacho hupendi kuona ukifa nacho bila kukufanyia kazi?
Ikiwa kuna wazo au kitu cha kufanya leo kwa nini usifanye kitu hicho ili kukusogeza kwenye ndoto zako kuliko kuendelea kusubiri?
Je, unajua kitu kinachokuzuia wewe na watu wengine pia kuchukua hatua za haraka kuelekea kwenye ndoto zao?

Chukua hatua mapema.
Woga.
Kitu gani hasa kinachokufanya ushindwe kuchukua hatua za kutimiza ndoto zako? Unaogopa utashindwa. Unaogopa ikiwa utafanya halafu ukashindwa kufanikiwa utachekwa na watu.
Wengi utakuta wanaogopa mambo mengi ambayo kiuhalisa yanawarudisha nyuma na kuua ndoto zao kabisa. Woga ni sumu kubwa sana ya mafanikio kwa wengi.
Hatua za kufanya kuondoa woga huu.
Hakuna dawa nyingine ya kushinda woga unaokuzuia ushindwe zaidi ya kuchukua hatua mapema za kuelekea kwenye ndoto yako.
Kila nafasi unayoipata itumie vizuri kuhakikisha ndoto na mipango yako inatumia wakati ukiwa una nguvu.
Ila ukisubiri sana mambo yameharibika ndio uanze kuchukua hatua utakuwa ni sawa na mtu ambaye anajichelewesha yeye mwenyewe.
Tekeleza ndoto na mipango yako kwa malengo huku ukichukua hatua mapema. Usiruhusu kufa na ndoto zako fanya mambo yako mapema.
Endelea kujifunza kupitia dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Kama makala hii imekusaidia na unapenda kujifunza zaidi, karibu kwenye kundi la Whats App ili tuweze kujifunza pamoja tena kwa ukaribu. Kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S, kisha ikifuatia na jina lako kwenda 0713 048035 ili uanganishwe.
TUNAKUTAKIA KILA LA KHERI KATIKA SAFARI YA MAFANIKIO.
Ni wako rafiki,
IMANI NGWANGWALU,

No comments :

Post a Comment