Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Thursday, January 12, 2017

Unapokosa Hamasa Ya Kile Unachokifanya, Kumbuka Mambo Haya.

No comments :
Katika maisha kuna wakati mwingine pamoja na kuweka juhudi nyingi sana kwa kile kitu unachokifanya tena kwa muda mrefu lakini unakuwa bado hupati matokeo ya kile unachokitaka.
Kwa mfano, utakuta umeweka juhudi kubwa kwa jambo fulani tena kwa muda mrefu , lakini hauoni mafanikio makubwa sana. Kwa hali kama hii hukupelekea moja kwa moja kuanza kukosa hamasa na kukata tamaa.
Kukosa huko hamasa na hali ya kukata tamaa huanza kujitokeza hasa pale unapoona wale ambao wanafanya jambo hilohilo tena wakiwa wameanza muda si mrefu wakifanikiwa.
Wengi wanapokutana na hali kama hiyo ile hamasa ya kufanya jambo hilo hupungua sana siku hadi siku na mwisho hujikuta kabisa wameachana na jambo hilo kwa kuona eti haliwafai.
Sasa basi kila wakati kumbuka hamasa ndio chachu kubwa ya kuweza kukufikisha kwenye mafanikio yoyote yale. Kwa maana hiyo ninachotaka kukwambia kila unapokosa hamasa  kumbuka sana mambo haya.
1. Tambua vizuri sababu za kuanza jambo hilo.
Sina shaka kabisa zipo sababu ambazo zilipelekea ukaanza hicho unachokifanya. Hebu fanya zoezi la kuziandika sababu hizo na kuzipitia kila wakati.
Kwa jinsi utakavyokuwa unazipitia sababu hizo ni rahisi sana kukupa hamasa upya na kuona haipo sababu ya kukata tamaa kama sababu zako zinajitosheleza.
Kwa mfano, pengine ulianza jambo hilo ili kuwasaidia wengine. Kama iko hivyo, hiyo ina maana kukosa kwako hamasa na kukata tamaa kutapelekea hao wengine usiwasaidie.
Kabla hujakata tamaa kumbuka ulikotoka.

Hivyo, dawa ya kurudisha hamasa hapo ni kwa wewe kuendelea kufanya hata kama matokeo hupati mazuri. Kupitia kujifunza tena na kujua sababu kwa nini ulianza zitapelekea wewe kufanikiwa.
2. Hakuna mafanikio kama unakata tamaa mapema.
Inawezekana unakosa hamasa kwa sababu hupati matokeo ya haraka. Unachotakiwa kukikumbuka hapa mapema ni kwamba Kufikia mafanikio yoyote inahitaji juhudi na nguvu nyingi tena sio kwa muda mfupi.  
Hakuna mafanikio ambayo unaweza kuyapata kama unakata tamaa mapema. Weka juhudi zako kwa muda mrefu huku ukijua kupata mafanikio itakuwa ni lazima kwako na itakuwa hivyo.
3. Acha kujishusha.
Hata kama hupati matokeo makubwa kama wengine wanayoyapata kwenye jambo unalolifanya lakini kitu kikubwa cha kuangalia acha kujidharau na kujishusha kabisa.
Unaweza tena kufanikiwa ikiwa utatumia njia nyingine na kujaribu tena. Mafanikio yanakuja kwako sio mara moja bali ni kwa kufanya tena na tena mpaka unapata matokeo chanya.
4. Tafuta msaada.
Pia kama unaona hamasa unaikosa kabisa ni vyema ukatafuta msaada hasa kwa kuwangalia wale waliofanikiwa kwa kiasi kikubwa hasa kwa hilo jambo ambalo unalifanya sasa.
Kwa kuzingatia mambo hayo yaani kujua sababu zilizokufanya ukaanza jambo hilo unalolifanya, kuacha kujishusha na kutafuta msaada ni moja ya mambo yatakayokusaidia kurudisha hamasa ya mafanikio yako upya.
Endelea kujifunza kupitia dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Kama makala hii imekusaidia na unapenda kujifunza zaidi, karibu kwenye kundi la Whats App ili tuweze kujifunza pamoja tena kwa ukaribu. Kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S, kisha ikifuatia na jina lako kwenda 0713 048035 ili uanganishwe.
TUNAKUTAKIA KILA LA KHERI KATIKA SAFARI YA MAFANIKIO.
Ni wako rafiki,
IMANI NGWANGWALU,

No comments :

Post a Comment