Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Monday, January 9, 2017

Ili Ufanikiwe, Unahitaji Kuondoa Mambo Haya Kwenye Maisha Yako Kabisa.

No comments :
Ili uweze kufanikiwa upo ulazima wa wewe kuongeza maarifa na tabia mpya za mafanikio kila kukicha. Hili ni hitaji la msingi sana kwa mtu yeyote ambaye ana nia ya kufikia mafanikio makubwa maishani mwake.
Pamoja na ukweli huo ambao hauwezi kupingwa,  lakini pia upo ulazima wa kuondoa tabia mbaya zinazokukwamisha katika safari ya mafanikio. Tabia hizi mbaya ni lazima kuziondoa ili kuzifanya mpya zifanye kazi vizuri.
Hautaweza kufanikiwa ikiwa kila wakati unaongeza tabia mpya za mafanikio na kusahau kutoa zile tabia mbaya zinazokukwamisha kwa namna moja au nyingine katika maisha yako.
Najua zipo tabia ambazo kwa kawaida zinaturudisha nyuma sana kwenye mafanikio yetu. Hizo ndizo tabia ambazo unatakiwa uziangalie kwa ukaribu na kuziondoa mara moja kwenye maisha yako.
Kuendelea kuzing’ang’ania tabia hizi ambazo ni hasi, ni sawa na wewe mwenyewe kuamua kujitengenezea njia au kushindwa kwenye maisha yako mwenyewe, hivyo ni muhimu sana kuzibadili.
Unataka kujua zaidi ni tabia zipi mbaya unatakiwa kuziondoa, fuatana nami katika makala haya nikuangazie nukta kadhaa zitakazokusaidia moja kwa moja kuweza kuondoa tabia ambazo ni sumu kwa mafanikio yako.
1. Ondoa visingizio.
Jifunze kuwajibika kwenye maisha yako kwa asilimia zote. Kama kuna jambo umeshindwa kulifanya kubali tu umeshindwa ila acha visingizio. Kuendelea kuwa na visingio kila siku hakutakusaidia kitu chochote.
Watu wenye mafanikio kila wakati ni watu wa kuwajibika. Hakuna kitu ambacho wanasingizia kwamba kimewakwamisha zaidi yao wenyewe. Ukielewa hili, litakusaidia kupiga hatua na kupelekea kuchukua hatua.

Ondoa woga kwenye maisha yako, ili kujihakikishia mafanikio makubwa.

2. Ondoa woga.
Hautaweza kufanikiwa kama ndani yako kila wakati umejaa na woga. Unapokuwa na woga inakuwa inakufanya ushindwe kujaribu mambo mengi ikiwa pamoja na fursa zinazoweza kujitokeza. Hakikisha leo unakula kiapo cha kuondoa woga ili uweze kufanikiwa mara moja.
3. Ondoa wazo la kufanikiwa upesi.
Mafanikio yote siku zote ni mipango. Mafanikio yanakuja hatua kwa hatua. Sasa kama una wazo la kutaka kufanikiwa kwa haraka bila kuwa na subira, huku unakoelekea ni kubaya. Jiwekee mipango, itekeleze kila siku, utafanikiwa. Hakuna mafanikio ya kulala maskini, na kuamka tajiri. JIPANGE.
4. Ondoa watu hasi.
Maisha yako yatakuwa ya mafanikio kama utakaa mbali na watu hasi. Watu hasi ni sumu kubwa sana ya mafanikio yako. Hawa ni watu ambao watakukatisha tamaa na kukufanya ushindwe kufanikiwa. Kwa hiyo, ni lazima sana kwako wewe kuweza kukaaa nao mbali ili kujihahakishia mafanikio.
5. Ondoa tabia ya kukubali kila kitu.
Epuka sana kuwa mtu wa kukubali kila kitu, hata pale ambapo hutaki kitu fulani. Unapokuwa ‘Mr. Yes or Mrs. Yes’ kila wakati ni hatari sana kwa mafanikio yako kwa sababu kuna wakati utajiingiza kwenye makubaliano ambayo hukuyataka.
6. Ondoa mawazo mgando.
Kila wakati kuwa mtu wa kutaka vitu vipya. Zile fikra zako kuhusiana na jambo fulani jaribu kuzipima kila wakati, je, kwamba zinakusaidaia kuweza kufanikiwa? Ukitoa mawazo mgando maishani mwako, utajua mambo mengi na pia itakuwa ni njia rahisi ya kufanikiwa kwako.
Kumbuka kila wakati kutoa tabia mbaya zinazokukwamisha ni jambo ambalo unatakiwa kulichunguza sana, ili kuweza kufikia mafanikio yako.
Uwe na wakati mwema na siku njema katika harakati zako za kufikia mafanikio makubwa.
Endelea kujifunza kupitia dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Kama makala hii imekusaidia na unapenda kujifunza zaidi, karibu kwenye kundi la Whats App ili tuweze kujifunza pamoja tena kwa ukaribu. Kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S, kisha ikifuatia na jina lako kwenda 0713 048035 ili uanganishwe.
Ni wako rafiki,
IMANI NGWANGWALU,
dirayamafanikio.blogspot.com  

No comments :

Post a Comment