google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Jan 2, 2017

Siri Ya Mafanikio Yako Mwaka 2017.

No comments :
Habari za muda huu mpenzi msomaji wa makala hii ya DIRA YAMAFANIKIO. Siku ya leo ningependa kuchukua fursa hii niweze kukushirikisha mambo mbalimbali ambayo yataweza kukuondoa kutoka sehemu moja hadi nyingine ya kimafanikio hasa mwaka huu wa 2017.
Kwa kawaida yapo mambo mbalimbali ambayo unaweza ukajifunza binafsi hata pia kupitia watu waliofanikiwa. Mafanikio ya kimaisha huja kwa kuiweka akili yako kuweza kupambana na changamoto za kimaisha na hatimaye kuona mwanga wa mafanikio. 

Naamini una kiu kubwa ya kutaka kuona mwaka 2017 ukiisha ukiwa na mafanikio makubwa. je, unajua siri ya mafanikio yako kwa mwaka 2017 iko wapi? 

1. Tazama fursa zilizopo.
Mpenzi msomaji wangu wa makala hii jitahidi kuzitazama fursa zilizopo katika eneo lako unaloishi au nje ya eneo lako unaloishi. Fursa zilizopo ni chanzo kikubwa cha utajiri wa kimafanikio. Nasema hivi ni kwa na maana ya kwamba fursa mara nyingine hutoka na changamoto zilizopo eneo fulani, fursa hizi huenda zikawa aina mbalimbali za mahitaji ya watu.
Ikiwa bado hujanielewa vizuri naomba nikupe mfano huu. Tuchukulie  mtaani kwako kuna tatizo la eneo la kutupa taka taka unaweza ukachukua kama fursa hiyo na kuanza kupita kwa makazi ya watu na kuchukua taka hizo na kwenda kuzihifadhi eneo husika na hatimaye wakazi hao kukulipa kiasi cha fedha . Na vilevile kila changamoto zilizopo eneo furani ni fursa ya kuweza kupata kipato na hatimaye kuona fursa ya mafanikio.

2. Jiamini wewe mwenyewe.
Mafanikio yote makubwa huja kutokana na kujiamini wewe mwenyewe na kuua hofu zote zinazokukwamisha. Unapojiamini unajijengea nafasi nzuri sana ya kufikia mafanikio yako makubwa. Ni muhimu sana kuweka jitihada zako wewe mwenyewe kuwa unaweza kufanikiwa huku ukijiamini. Hata kama unachukua ushauri kwa wengine ni jambo zuri sana lakini kikubwa jiamini.
Ili uweze kuongeza uwezo mkubwa wa kujiamini ni vyema kuwa na mawazo chanya yenye kuleta maono ya kufanikiwa hapo baadae. Hakuna dhambi kubwa kama kukata tamaa jiamini kuwa unaweza ama hakika utafanikiwa maisha siyo magumu kihivyo kama wengi tunavyofikiri ila sisi ndio wagumu na daima siku zote kitu rahisi ndicho sahihi.
3. Acha kusikiliza maneno ya watu wanaokukatisha tamaa.
Wapo baadhi ya watu ambao wapo kwa ajili ya kuwakatisha watu wengine tamaa. Hivyo basi kama wewe ni kweli unahitaji mafanikio najua yapo mengi yatasemwa juu yako kwa ajili ya kukuvunja moyo. Wewe wasikilize tu watu hao lakini achana na mawazo hasi ambayo hayana tija kimafanikio na sumu kubwa kwako.
Siku zote jifunze kuwa ni mtu wa kusikiliza mawazo chanya yenye kuleta njia sahihi ya kuona maono ya kimafaniko. Kuwa makini katika kuchagua marafiki sahihi wenye mawazo yakinifu yenye kuleta mtazamo wa kimafaniko. Achana na watu wataokurudisha nyuma kimafanikio kwa namna yoyote ile.
4. Kukabiliana na changamoto zinazojitokeza.
Tambua ya kuwa hakuna mafanikio yasiyo kuwa na changamoto.Hivyo jitahidi kuwa ni mtu kukubaliana na changamoto hizo na kujua namna utakavyoweza kukumbana na changamoto hizo .Usiwe ni mtu wa kukata tamaa sana.
Vile vile siri kubwa ya mafanikio ni kujifunza na kutokuogopa kujaribu. Hautaweza kufanikiwa kwa kukaaa tu na kutokuwa mbunifu na jinsi ya kupambana kimaisha na changamoto za kimaisha na hatimaye kufanikiwa. Hakikisha unafanya kazi kwa biidii ili malengo yako yaweze kutimia.
5. Fanya kazi kwa bidii.
Hiyo ni nguzo kubwa katika mafanikio. Hakikisha unajituma zaidi katika kufanya kazi.Tumia muda wako vizuri na kwa mapangalio mzuri ili kuhakikisha unapata mafanikio unayoyahitaji. Tumia ujuzi,nguvu na maarifa uliyonayo katika kufanya kazi.
Ifanye kazi iwe ndiyo msingi wa mafanikio yako. Mara kwa mara inapotokea unakosa hamasa ya kufanya kazi, jipe hamasa na kuendelea kuchapa kazi bila kuchoka. Ukichukua tabia hii, mafanikio makubwa yatakuwa upande wako. Hii ni siri nzuri sana ya kukufikisha kwenye mafanikio makubwa.
6. Simamia maono yako.
Hakikisha unasimamia malengo yako uliyojiwekea ili kuona ndoto zako zinatimia kwa muda muafaka. Maono ni malengo yako ambayo wewe mwenyewe umejiwekea ambayo utapenda kuyatimiza hapo baadae na kuona unayaona mafanikio. Kumbuka kufanya tathmini ya malengo yako ni wapi ulishindwa kutimiza malengo yako, na utaweje kukumbana na changamoto hizo na hatimaye kutimiza malengo yako.
Kwa kujifunza mambo hayo itakusaidia sana wewe kuweza kufikia mafanikio makubwa uliyojiwekea katika maisha yako kwa mwaka 2017..
DIRAYA MAFANIKIO inakutakia kila la kheri katika safari yako yako ya kuelekea kwenye mafanikio.
Makala hii imeandaliwa na:-
Afisa mipango na mendeleo,
Mr. Benson o. Chonya,
Mawasiliano,
Instragram; Benson Chonya,
Twitter; @bensonchonya,
Facebook; Benson Chonya,
Whatsapp; 0757 90 99 42.





No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.