Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Saturday, January 14, 2017

Jitofautishe Na Wengine Ili Ujenge Mafanikio Makubwa.

No comments :
Kufikia mafanikio makubwa kwa mujibu wa tafiti nyingi zinaonyesha ni matokeo ya kufanya jambo lilelile ambalo pengine  kila mtu analifanya lakini kwa njia tofauti. Hakuna uchawi tofauti na huo wa kufanya jambo lilelile lakini kwa utofauti.
Kama unajidanganya unasema mazingira mabovu ndiyo yanayokufanya uwe na hali ngumu unajidanganya. Katikati ya hayo mazingira mabovu kuna watu waliofanikiwa sana, na bila shaka hata wewe ni shahidi wa hilo na unawajua.
Kama unasema ‘oooh mimi sijafanikiwa kwa sababu sina kipaji au uwezo wangu ni mdogo pia unajidanganya.’ Dunia ina watu wengi sana ambao wanamafanikio makubwa  lakini hawakuwa na uwezo kama huo mkubwa unaofikiri.
Kama pia unasema mimi sifanikiwi kwa sababu sifanyi biashara ya aina fulani pia unajidanganya. Hakuna biashara ambayo ukiifanya ni lazima uwe tajiri moja kwa moja, nasema biashara hiyo haipo.
Watu ni matajiri katika kila biashara. Kama unafikiri natania angalia mtaani upate ushahidi kamili. Ile biashara unayoidharau kuna mwingine ni tajiri kupitia hiyo biashara ambayo unaiona haifai.

Fanya mambo yako kwa utofauti mkubwa ili upate matokeo mazuri.
Hakuna mtu ambaye ameshindwa kuufikia utajiri eti kwa sababu hana mtaji. Na hakuna mtu ambaye ana mtaji na akajihakikishia utajiri wa moja kwa moja. Kinachokupa mafanikio ni kwa jinsi wewe unavyofanya vitu kwa utofauti.
Haijalishi wewe ni maskini kiasi gani kama unafanya mambo yako kwa utofauti ni lazima kwa vyovyote vile utatoka huko kwenye dimbwi la umaskini na kuanza kuupata utajiri polepole.
Unataka kufanikiwa fanya mambo yako kwa njia tofauti. Unaweza ukawa ni mkulima sawa, lakini lima huku ukiongeza ubunifu na kujua ni kipi cha ziada ambacho kinaweza kuongeza mazao yako thamani.?
Kama wewe ni mfanyabiashara fanya biashara yako huku ukiongeza ubunifu wa hali ya juu sana kila siku. Jifunze kwa wafanyabiara wenzako na pia jifunze kupitia semina mbalimbali.
Utafika mbali sana kimafanikio na kuwa mtu wa tofauti ikiwa utajua na kujifunza kufanya mambo yako kwa utofauti. Kila wakati jifunze kutafakari na kutambua je, unafanya mambo yako kwa utofauti?
Kama ni mtu wa kuiga iga na kusahau kabisa kufanya mambo kwa utofauti  ni kuhakikishie kabisa sahau kitu kinachoitwa mafanikio makubwa. Mafanikio makubwa yanajengwa na wewe kwa  kuwa watofauti.
Naomba usije ukanielewa vibaya simaanishi uanze kufanya jambo jipya kabisa hapana. Fanya jambo lilelile, lakini lilokubwa kwako kumbuka kufanya kwa utofauti. Hapo ndipo siri kubwa ya mafanikio ilipo.
Kwa hali yoyote uliyonayo unaweza kubadili maisha yako na kuwa mtu wa tofauti kabisa ikiwa utakuwa unatenda kwa utofauti. Kama ulikuwa huna mtaji, upo kwenye madeni vitu vyote hivyo utavipata na kufikia mafanikio yako.
Nimalize makala haya kwa kusema hivi, kupata utajiri hakutegemei sana mazingira, hali, kipaji au unafanya biashara ya namna gani. Bali kupata utajiri kunategemea sana je, vitu hivyo unavyovifanya una vifanya kwa utofauti?
Endelea kujifunza kupitia dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Kama makala hii imekusaidia na unapenda kujifunza zaidi, karibu kwenye kundi la Whats App ili tuweze kujifunza pamoja tena kwa ukaribu. Kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S, kisha ikifuatia na jina lako kwenda 0713 048035 ili uanganishwe.
TUNAKUTAKIA KILA LA KHERI KATIKA SAFARI YA MAFANIKIO.
Ni wako rafiki,
IMANI NGWANGWALU,
No comments :

Post a Comment