google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Mar 1, 2016

Ukiyafanya Haya, Mafanikio Makubwa Yapo Upande Wako.

No comments :
Kwa muda mrefu umekuwa ukijiuliza ni vipi utapata mafanikio unayoyahitaji?  Lakini jibu ni kwamba mafanikio unayo wewe mwenyewe ila tatizo ni kwamba unakuwa ni mtu wa kusuasua kuanza mambo hayo ya kusaka mafanikio.
Ngoja nikukumbushe ya kwamba hakuna muda maalumu wa kuyasaka mafanikio. Utawasikia watu wengine wanasema eti nikiwa au ukifika miaka 35 au 40 eti ndo utaanza kuyasaka mafanikio kwa kuwa na nyumba, magari na mengineyo.
Hii sio kweli  kumbuka ya kwamba muda wa mafanikio ni sasa na wewe ndio mwamuzi wa kuamua  kuanza kuchangamkia fursa zilizopo ili uweze kuwa miongoni  mwa matajiri ambao utakuwa unatajwa midomoni  mwa watu,  naamini  ya kuwa unaweza.
Wapo baadhi ya matajiri wakubwa tunaowajua. Leo ukijaribu kusoma historia zao wengi wameanza kuwa na mitaji midogo kabisa  lakini leo hii ndio ambao wapo midomoni mwetu na pengine tumekuwa tukishangaa sana mafanikio yao.
Kwa sisi ambao bado hatujapata mafanikio, kwa muda mwingi tunakaa vijiweni tunawajadili , kuwasifia na kuwapa sifa nyingi nzuri bila wao kutusikia hata kutujua majina yetu,  huku wao wakiingiza  fedha na kuzidi kutajirika zaidi.
Kiuhalisia, yapo baadhi ya mambo ambayo leo hii tukiyafanya , sisi  wengine ambao hatuna siri hii ya utajiri,  tukiijua vizuri tutakuwa kama wao. Sasa twende pamoja kujifunza baadhi ya mambo ambayo leo hii ukiyafanya mafanikio makubwa yatakuwa upande upande wako.
Jambo la kwanza; Tenga muda wa kufikiri mambo yako.
Muda ni jambo la msingi sana katika safari ya mafanikio. Kisaikolojia binadamu wote ni sawa ila tunatofautina sana  katika matumizi ya muda. Ngoja nikupe mfano huu ili uweze kunielewa zaidi.  Kwa siku kuna masaa 24. Masaa haya jinsi anavyotumia masikini na tajiri ni tofauti kabisa. Tajiri masaa haya huyaona hayotoshi kwa sababu ana mambo mengi ya kufanya. Ndio maana hata baadhi ya matajiri ukiwa hufanyi vizuri katika kazi zao utawasikia wanasema usinipotezee muda  maana kwao muda ni mali.
Lakini masaa hayohayo kwa maskini huwa ni masaa mengi sana kwa sababu hana mambo mengi ya kufanya hata kufikiria pia. Maskini huyohuyo akitaka kuamka asubuhi utamsikia anauliza hivi jua limechomoza. Kwa maana ya kwamba yeye huongozwa kwa kulitazama jua. Halikadhalika akiamka asubuhi utamsikia usiku wa leo ulikuwa mrefu sana. Ewe  msomaji wa makala haya ukifanya hivyo mafanikio utayasikia kwa akina Bill Gate tu.
BADILI RATIBA YA KUFANYA MAMBO YAKO.
Jambo la muhimu kumbuka ya kwamba kama kweli umechoka na hali ya umaskini hakikisha unatenga muda wa kufikiri mambo ya mafanikio kila siku.  Wakati upo katika muda wa kufikiri mambo yako ya kimafanikio hakikisha ya kwamba unakaa sehemu tulivu ambazo hazina kelele za aina yeyote ile kama vile watoto,  simu, radio, televisheni na sauti zingine ambazo zitakufanya ufikilie vizuri mambo yako ya muhimu.
Pia kumbuka wazo zuri ambalo utalipata wakati umetenga muda wa kufikiria mambo yako, lifikirie mwanzo hadi mwisho wa jambo hilo. Pia liwe ni jambo moja. Liandike kwenye karatisi au mahali popote ambapo unahisi hatapasau kwa urahisi yaani ikiwezekana iwe sehemu inayoonekana.
Andika mikakati mizima ya utekelezaji wa jambo hilo. Kwa kuangalia zana ambazo zitatumika kuangalia jambo hilo, pia jaribu kutazama changamoto ambazo unahisi zitajitokeza juu ya jambo hilo pamoja na jinsi ya kukabiliana changamoto hizo na jaribu kuona matokeo ya jambo hilo. Kwa ufupi lazima uone maono (Vision) ya wazo lako.
Jambo la pili; badili ratiba ya kufanya mambo yako.
Kuna baadhi ya watu tunafanya vitu kimazoa sana hii inapelekea  siku zote tunabaki  vilevile huku tukilalamika ya kuwa maisha ni magumu. Tukumbuke ya kwamba Kufanya vitu kimazoea kunamfanya mtu asiweze kusongo mbele.
Watu wengi ambao wanalamika juu ya maisha asilimia kubwa utagundua ya kwamba wanafanya vitu kimazoea.  Kama kweli unapenda jambo fulani la kimafanikio, basi usilifanye  kwa mazoea.  Fanya vitu tofauti na ulivyozoea utaona matokeo makubwa ya kimafanikio yapo upande wako.
Kama umezoea kuamuka saa mbili kamili asubuhi basi amka saa kumi na mbili asubuhi ili uone mpaka saa mbili utakuwa umefanya nini, kama umezoea kufunga biashara yako saa tatu usiku basi ongeza muda wa kufunga biashara yako hadi saa tano ili uwone kama kuna mabadiliko. Kama wewe ni mvivu basi anza kuwa miongoni mwa watu wanaofanya kazi kwa bidii.
Endapo utafanya hayo yote kwa kuzingatia wewe ni msaka tonge mafanikio makubwa yapo upande wako. Usikate tamaa katika kila jambo unalolifanya. Kuwa shupavu kama simba,  maana simba akikosa nyama hawezi kula nyasi atapambana huku na huko ili apate nyama.
Kama una maswali , ushauri au mapendekezo usisite kuwasiliana na afisa maendeleo na mipango, mwandishi wa makala haya  Benson Chonya.  Usisite pia kumshirikisha mwenzako ili aweze kujifunza pia.
Simu; +255 (0) 652 015 024

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.