Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Monday, March 28, 2016

Mambo Mawili (2) Yanayotukwamisha Kufikia Malengo Yetu.

No comments :
Yapo mambo mengi ambayo umekuwa ukiyaona au kuyasikia ambayo yanakufanya usonge mbele au kurudi nyuma katika safari yako mafanikio.  Jambo la msingi ni jinsi gani ambavyo unachukulia mambo hayo  katika kuoziona fursa katika eneo lako unaloishi. Lakini  katika makala ya leo tunakwenda kujikita zaidi kwa kuangalia mambo ambayo yanatufanya tuzidi kuwa wanyonge na kuona mafanikio ni ya watu wachache.
Yafuatayo ni baadhi ya mambo yanayotukwamisha kufika malengo.
JAMBO LA KWANZA.
Kusemwa na  watu juu ya jambo lako. Tunashindwa kufika malengo makubwa kwa sababu , sisi wenyewe ni kikwazo katika baadhi ya mambo  ambayo hayana msaada wowote wa kimafanikio kwa watu wengine.  Wapo baadhi ya watu wapo  kwa ajili ya kuona watu  wengine hawasogei mbele kimafanikio .  Wao wamekuwa na maneno ya kuwakatisha watu wengine tamaa kwa kuwaambia wahusika maneno ambayo hayawajengi bali yanawarudisha nyuma. Mfano leo hii anamwambia mtu unataka kufanya biashara fulani, mtu huyo atakwambia hataweza kufanya jambo hilo kwa kuwa hufanani na kitu hicho unachotaka kufanya.
Wapo baadhi ya watu ukiwashirikisha mambo yako wao huchukua hatua ya kuwashirikisha watu wengine na kuwambia  fulani anataka kufunya jambo fulani. Lakini jambo la msingi la kuzingatia ili kuona unapata faida katika jambo lako unalofanya hakikisha maneno ya watu wanayokusema yanakupa hamasa za kiutendaji na kuongeza juhudi ili kupata faida kubwa.

JIAMINI KWA KILE UNACHOKIFANYA.
Mfano wewe ni mfanyabiashara watu wanakusema wewe unafanya biashara kwa njia za ushirikina au maneno mengine yanayofanana na hayo achana na maneno hayo bali songa mbele kwa kuziona fursa za jambo lolote ili kupata faida kubwa. Watu wanapozidi kukusema wewe unazidi kufanikiwa zaidi.
JAMBO LA PILI
Kusubiri kuambiwa ufanye jambo fulani. Hili ni jambo linalotukwamisha sana katika safari ya mafanikio. Watu wengine tunapenda kufanya mambo ya kimafanikio kwa kuambiwa na mtu mwingine. Wengi tunasubiri kuambiwa fanya hiki au fanya kile. Katika safari ya mafanikio  ukisubiri kuwaambiwa na mtu fanya hiki au fanya kile kwa upande wako mafanikio yatakuwa ni ndoto tu.
Mfano wewe ni mwanafunzi unasubiri mwalimu wako mpaka akuambie kasome kitu fulani au wewe ni mfanyabiashara unasubiri mtu akwambie boresha ofisi yako ili kuongeza wateja  ila wewe kwa akili yako hata siku moja hujawahi kujipa kazi za kufanya au kujiuliza ufanye nini ili kuboresha biashara. Kimsingi kufanya hivi ni sawa na kumfunika nyoka kwenye tenga ili asitoke.
Ewe msomaji wa makala haya ili kuona unafanikiwa kwa kiwango kikubwa hakikisha kwa kila jambo unalolifanya usisibiri mtu  fulani akwambie ufanye bali kuwa na akili ya kujiongeza. Kufanya hivi kutakufanya kuongeza ufanisi wa kiutendaji na kupata kile unachokihitaji.
Ansante kwa kutembelea DIRA YA MAFANIKIO na endelea kuwashirikisha wengine kujifunza zaidi.
Makala hii imeandikwa na afisa mipango na maendeleo; Benson chonya
Simu; 0757-909942

Email ; Bensonchonya23@gmail.com

No comments :

Post a Comment