Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Wednesday, March 2, 2016

Siri Iliyopo Kati Ya Mafanikio Na Mwonekano Wako.

No comments :
Habarini za leo mpendwa msomaji wa DIRA YA MAFANIKIO. Karibu tena katika siku nyingine ya kuweza kujifunza. Leo katika somo letu tutazungumzia haiba ya mtu au mwonekano wa mtu katika kuleta mafanikio. Nawaletea siri iliyoko katika mwonekano wa mtu na uhusiano wake katika mafanikio.

Thamani ya mtu haiko katika mwonekano wa nje tu. Vipo vingine vya ndani vinavyoweza kumwonesha mtu haiba au mwonekano wake na kuwa eidha chanzo cha mafanikio au kutofanikiwa kwake. Mafanikio ya  binadamu yanaanzia kwenye thamani aliyonayo kwa binadamu wenzie.

Mwonekano wako unaweza kukuweka katika daraja la juu au kukushusha daraja na hata thamani kwa watu. Tabia ya mtu inaweza kubadilika lakini haiwezi kubadilishwa. Hapa najua wengi nimewaacha njia panda. Ni kuwa tabia ya binadamu anaweza kuibadili mtu mwenyewe kwa kuamua kubadilika na sio kuamuliwa na mtu abadilike.

Kuamua kubadili tabia ni uamuzi wa mtu mwenyewe lakini  kubadilishwa tabia ni hatua nyingine ni rahisi kurudia asili yake. Kila binadamu amezaliwa ili afanikiwe na kila binadamu ameumbwa kwa makusudi maalumu. Hakuna ambae ameletwa duniani bila ya kusudi maalumu.

TEMBEA YA MTU INAONYESHA MAFANIKIO YAKE
Lakini ukweli ni kwamba 90% ya watu wanaishi, ingawa hawajui makusudi ya kuwepo kwao duniani na ndio maana tunaishi maisha ya kubahatisha. Tunasoma elimu kubwa lakini mafanikio kidogo, tunasomea udaktari wakati, tunauwezo mkubwa katika mahesabu, tunasoma kilimo wakati tunapenda kufundisha na mengineyo mengi.

Hii yote binadamu anafanya kwa sababu ya kutojua kusudi lake la kuumbwa na kuwepo duniani. Mzee wa nyundo nakuhabarisha leo. Ni namna gani utajenga haiba yako na kutambua kusudi lako hapa duniani? Fuatana nami nikupe siri ya mafanikio leo. Nataka nikupe siri ambayo itakuangazia pale penye Giza. Mwalimu wangu wa saikolojia aliwahi kuniambia hata mwandiko wa mtu hujulisha tabia yake aliyonayo. Tukacheka lakini baadae alituthibitishia ukweli wa kauli yake na leo nakufahamisha nawe vitu vinavyoonyesha tabia na haiba ya mtu.

1. Mavazi, mavazi yanamshepu mtu na kutoa thamani au kupunguza thamani ya mtu. Vile unavyovaa inatoa mwonekano wako ulivyo.

2. Kauli au mazungumzo ya mtu,  hili halina ubishi ukiongea na mtu mkorofi au mpole na mwenye hekma utajua tu.

3. Tembea ya mtu, kila mtu anatembea yake lakini kila tembea ina ishara yake kimwonekano. Mtu mwenye dharau hutembea kwa maringo na mtu anaejiamini hutembea mwendo wa haraka  najua hapa utahoji ndio ni kweli.

 4. Kujibu au kuuliza  kwako maswali nayo huonyesha tabia yako kwa urahisi sana kuwa ni mwema au unadharau, unajiamini au hujiamini.

5. Kula kwako nako kunaonyesha ni mlafi au mkarimu. Hizi ni moja ya tabia au mwonekano wa mtu ambao kwa namna moja au nyingine unaweza kumpelekea mtu kuaminiwa na wengine na kupata mafanikio au kutoaminika na kukosa mafanikio.

Kila tabia ina faida na hasara zake pia. Saikolojia inatuaminisha kuwa tabia ya mtu ya nje ndio tabia yake ya ndani. Ni ngumu sana mtu kuigiza tabia asiyokuwa nayo ndani mwake labda aamue kubadilika kabisa mwenyewe na kuachana na tabia yake ya awali.

Tabia ya mtu kimafanikio au kutofanikiwa huanzia ndani mwake katika kufikiri, kuwaza na kutenda kwake. Kwa kumalizia somo letu ni tambua, binadamu sote tunaishi kwa Imani. Na Imani ndio pekee inayomfanya mtu eidha kufanikiwa au kutokufanikiwa katika maisha yake. Imani ndiyo inayotuongoza au kutupotosha katika kutimiza malengo yetu. Ili tuweze kufanikiwa katika maisha yetu hatuna hiyari tena ni lazima tubadili haiba au mwonekano wetu wa nje na ndani.

Inatakiwa pia tubadili tabia zetu katika kusema na kutenda. Tuwe na fikra chanya na kuacha kuishi kimazoea. Mafanikio ni haki yetu sote tukiamua inawezekana sana tena bila ya kutumia nguvu kubwa wala uchawi. Tuamue kuanzia leo kubadili Haiba zetu na kuishi kimafanikio tuweze kutimiza ndoto zetu na kufikia Uhuru wa kipesa na kiuchumi.

Kama una maswali , ushauri au mapendekezo usisite kuwasilliana na mshauri wa mafanikio, mwanasaikolojia na mwandishi wa makala haya Sharrif Kisuda alimaarufu Mzee wa Nyundo kali.  Lakini usisite kumshirikisha mwenzako ili aweze kujifunza pia kupitia mtandao huu wa DIRA YA MAFANIKIO kila siku.

Simu; +255 (0) 079 993

No comments :

Post a Comment