Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Tuesday, March 8, 2016

Hizi Ndizo Sauti (3) Zinazochangia Kuleta Mafanikio Yako.

No comments :
Mafanikio unayoyahitaji kesho msingi wake mkubwa huanzia leo. Ukitaka kufanikiwa inawezekana kabisa tena mara moja ndani ya sekunde kadhaa tu. Tupo baadhi yetu huwa tunajikatisha sana tamaa wenyewe kwa kujisemea baadhi ya maneno kama vile hivi nitaweza kweli? Maneno kama hayo yanakufanya uzidi kujiona wewe mnyonge na huwezi kusonga mbele siku zote. Kuna mwalimu wangu mmoja wa dini aliwahi kuniambia mdomo huumba kwa kile unachokisema ndicho kitakachokutokea, acha kujisemea maneno yenye kukutasha tamaa bali jinenee maneno ya ushindi siku zote.
Mara nyingi umekuwa ukisikika zaidi kuliko kusikiliza. Tofauti kubwa iliyopo kati ya kusikia na kusikiliza ni kama ifuatavyo, Kusikia ni kusikiliza kitu kwa juu juu tu bila kutilia umakini kwa kile unachokisikiliza mfano unasikia gari inatoa mngurumo, mtu atasikia sauti hii ile  lakini hata sikiliza. Ila kusikiliza ni kuwa makini kwa kile ambacho unasikiliza na kukielewa mfano mtu  akiamua kweli kusikiliza taarifa ya habari atakuwa makini na kuilewa na kinyume chake inawezekana pia.
Zifutazo ndizo sauti tatu zinazochangia mtu aweze kufanikiwa;
1. Sauti za watu tofauti tofauti.
Hizi ni zile aina na sauti ambazo umekuwa ukisikiliza kutoka kwa watu mbalimbali ambao wanakuzunguaka. Hizi ni sauti za watu zenye kukutia moyo ili uweze kuongeza juhudi kwa jambo unalolitaka ili uweze kufanikiwa. Wapo baadhi ya watu utawasikia wanasema ukijitahidi kufanya vitu fulani mfano katika masomo, biashara, kilimo na vitu vingine vingi utaweza kufanikiwa . Sauti hizi mtu huambiwa ili kumuongezea hamasa kwa kila jambo analofanya ili aweze kutimiza ndoto zako. Sauti hizi unaweza kusikia kutoka kwa watu waliofanikiwa hata wasiofanikiwa pia. Sauti hizi unaweza ukasikia katika semina na sehemu zinginezo.  Swali la kujiuliza  ni kwamba mafanikio yako yameletwa kwa njia hii au yataletwa kwa njia hii ya kuwasikiliza watu?

KUWA MAKINI NA KUSIKILIZA SAUTI ZINAZOKUZUNGUKA.
2. Sauti za historia mabalimbali.
Ni aina nyingine za sauti ambayo inachangia kwa kiwango fulani mtu aweze kufanikiwa. Sauti hizi za historia ni zile sauti ambazo tunasikia kutoka kwa watu mbalimbali ambao bado wanaishi au hatupo nao tena kwa  kusikia historia kwa baadhi ya mambo ambayo waliyafanya na bado wanayafanya  ili waweze kufanikiwa zaidi. Sauti hizi za historia tunazisikia kutoka kwa matajiri wakubwa kama vile wakina Bill Gate na wengineo wengi. Sauti na historia zao zinatufanya tuone ni jinsi gani walianza na leo hii wameweza kufanikiwa na kuwa matajiri wakubwa. Historia zao zinatufanya tujione na sisi tunaweza na siku moja tutakuwa au tutakuwa zaidi ya wao.
3. Isikilize sauti yako.
Hii ndiyo sauti kubwa kuliko sauti zote.  Sauti hii ni nyembamba sana ambayo ipo ndani ya moyo wa mtu . Watu wachache ambao wanaitambua sauti hii, Sauti hii humfanya mtu yeyote aweze kufanikiwa mara moja endapo utaamua kusikiza sauti yake.  Endapo utaamua kujitambua na kusikiza sauti hii ndio siku ambayo umaskini utakuwa umeupiga teke. Ngoja niendelee kukupa madini juu ya sauti hii, Kila mtu amekuwa na sauti hii nyembamba lakini anashindwa kuitumia hii ni kutoka na mfumo wa maisha ya kwamba huwezi kufanya kitu chochote mpaka  mtu fulani aamue juu ya maisha yako.
Ni watu wangapi leo wanafanya kazi kutokana na kusikiliza sauti za watu wengine kuliko kuzisikiliza sauti zao? Usinipe jibu. Ni watu wangapi leo hii wanajilaumu kwa kufanya kazi kwa ambazo hawazipendi hii ni kutokana walisikiza sauti za watu wengine? Ukichunguza kwa makini utagundua ni wachache mno wanaofanya kazi kwa upendo. Lakini ndugu msomaji wa makala haya kiukweli  sijui nikueleza vipi ili ujue sauti yako ndio ushindi wako ? Lakini tambua ya kuwa  siku ambayo utaamua kuisikilza sauti nyembamba  ambavyo inatoka moyoni mwako ndio siku ambayo utafanikiwa. Tukumbuke  bahati huja kwa waliojitayarisha.
Asante kwa kuendelea kufuatilia makala haya ya dira ya mafanikio
Makala hii imeandikwa na afisa mipango na maendeleo; Benson Chonya
Simu; 0757-909942

No comments :

Post a Comment