google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Mar 17, 2016

Jinsi Ya Kuweka Vipaumbele Hadi Kufikia Malengo Yako.

No comments :
Watu wengi sana duniani hawajui umuhimu na thamani ya kitu kuweka vipaumbele katika maisha yao. Mwanasaikolojia mmoja aliwahi kusema mtu yeyote anayeishi duniani akikosa Kipaumbele katika maisha yake hawezi kuishi atakavyo yeye bali ataishi watakavyo watu wengine. Nami nasema kama ukikosa kipaumbele katika maisha yako usubiri kuwa mtumwa katika maisha yako yote.

Tunapozungumzia vipaumbele ni dira au mwongozo unaomwongoza mtu  katika kutekeleza malengo aliyojiwekea. Kama tujuavyo kila binadamu ana malengo  yake katika maisha. Haijalishi ni madogo au makubwa ya muda mrefu au mfupi,mazuri au mabaya yote ni malengo.

Watu wengi tunashindwa kutimiza malengo yetu si kwa sababu hatuna elimu, si kana kwamba hatufanyi juhudi na hatuna moyo wa kufanya vitu vya maendeleo. Tumekosa kitu kimoja kidogo sana ambacho ni KIPAUMBELE. Kwa nini nasema tumekosa kipaumbele? Ngoja nikupe mfano.

Mwaka juzi nilikuwa natoa semina chuo kikuu cha Dar es salaam kuhusu Saikolojia ya namna ya kujitambua. Wakati naendelea na mada nilijaribu kuwauliza wanafunzi wa chuo mwaka wa pili je ukimaliza chuo utataka kufanya kazi gani itakayokulipa? au utataka kuwa nani ukimaliza chuo?

Majibu yaliyotoka utakubaliana na mimi kuwa watu hawana vipaumbele katika maisha yao. Moja ya wanafunzi anayesomea sheria alinijibu nataka kuwa mfanyabiashara mkubwa kama Bakheresa. Mwingine anayesomea shahada ya udaktari  alijibu mimi nataka nikimaliza chuo nataka niwe Pilot au rubani wa ndege kwa kuwa urubani unalipa sana mwaka moja tu nitakuwa tajiri. Mwingine akajibu mimi nikimaliza chuo nitafanya kazi yeyote ntakayoona inalipa na inaweza kunitoa kimaisha fasta. 

JIWEKEE VIPAUMBELE VYA KUWA MSHINDI.
Hao ndio wasomi wetu.Swali ni je hapa kuna mtu mwenye kipaumbele kitakacho mfikisha anapotaka? Jibu ni rahisi tu Wanachuo hawa wamekosa kipaumbele katika kutimiza ndoto zao. Wanajaribu kugusa kile kinachoweza kuwaletea mafanikio bila kujali ni kwa namna gani na kitaweza kumugharimu kiasi gani. Kumbuka siku zote kutambua na kuona ni vitu viwili tofauti.

Vipaumbele ni mwongozo ni hamasa zitakazo kufanya ujihimu na ujibidishe katika kuhakikisha unatimiza malengo ya ndoto zako. Vipaumbele vitakufanya usichoke kufanya kile unafanya kwa lengo la kuitimiza ndoto zako. Ukiwa na vipaumbele ni ngumu sana kukata tamaa na ni nguvu sana kufanya maamuzi tofauti na uliyokusudia. Ukiwa na vipaumbele hutapoteza muda wako bure kwa vitu ambavyo kamwe havita kusaidia ktk kutimiza ndoto zako. Alaaa kumbe! Kipaumbele ni kizuri sana mtu ukiwa nacho katika maisha eti eee!! Ansante sana mzee wa nyundo kwa kunihabarisha hili. 

Je nawezaje sasa kupanga vipaumbele vyangu katika maisha yangu ili nitimize malengo na ndoto zangu katika maisha? Twende pamoja mbona rahisi sana!

1. Kuwa na malengo katika maisha yako unataka kuwa nani katika uhai wako au siku za usoni kwa mbeleni. Unataka uwe mhandisi,injinia,daktari,mkulima au mfanyabiashara?

2.Unataka ufikie wapi kielimu chuo, kidato cha sita au unataka upate mwanga tu kisha usomee ujasiriamali?

3.Kiafya unataka uwe na unene kiasi gani au mwembana kiasi au mnene sana?

4.Kimaendeleo unataka umiliki vitu gani vya kifahari Nyumba, magari au nini unataka kumiliki?

5.Kiimani unataka familia yako,ndugu zako na  jamii kwa ujumla  ukitazamaje kuhusu Imani yako mtu wa Mungu,mnyenyekevu au katili na jeuri asie na upendo na watu? 

6. Kipesa unataka umiliki kiasi gani cha pesa ili kufikia malengo na furaha ya maisha yako. Hizi ni baadhi tu ya vipaumbele ambavyo unaeeza kujiwekea ktk maisha yako na vikakupa hamasa katika kutekeleza majukumu yako na kutimiza malengo yako uliyojiwekea katika maisha yako. Naomba kuishia hapa kwa leo nikutakie uwekaji mwema wa vipaumbele vitakavyo kuongoza kutimiza malengo yako.

Nikutakie siku njema na endelea kutembelea DIRA YA MAFANIKIO kwa ajili ya kujifunza kila siku.

Ni wako rafiki katika kusaka mafanikio ya kweli,

Shariff H. Kisuda alimaarufu mzee wa nyundo kali,
Simu; 0715 079993,
Email; kisudasharrif@gmail.com

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.