google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Mar 31, 2016

Hii Ndio Sababu Kubwa Ya Kushindwa Kufanikiwa Kwako.

No comments :
Mafanikio makubwa huja kwa watu waliojiandaa. Kitu hicho ni baadhi ya watu wachache sana ambao hutambua. Watu wengi tunafikiri ya kuwa mafanikio tunayoyahitaji msingi wake mkubwa ni mtaji kwa maana ya kuwa na pesa kwa ajili ya kuanzisha biashara au jambo lolote.

Kuwa na wazo hilo la kuwa na mtaji sio tatizo sana. Ila tatizo linakuja pale ambapo tunasahau ya kuwa kuna tatizo kubwa ambalo linafanya watu wengi washindwe kutimiza ndoto zao.

Jambo hilo ni WOGA BINAFSI hili ndilo tatizo kubwa ambalo watu wengi linawafanya washindwe kufikia ndoto Zao. Kuna usemi husema maisha ya mwanadamu yamethiriwa kwa kiasi kikubwa na woga.

Watu wengi wana woga wa uthubutu katika jambo fulani, mfano mtu leo hii anawaza katika akili yake kwamba hawezi kufanya jambo fulani. Akili yake ndivyo inavyowaza hii ni kutokana na woga alio nao katika nafsi yake.

Woga binafsi mara nyingine hujenga na jamii ya watu ambao wanakuzunguka. Mfano leo hii unataka kuanzisha biashara fulani kuna baadhi ya watu watakwambia hautaweza na wewe unaamini kweli hautaweza, hii ni kutokana umeshajenga woga binafsi kwa kuwa mtu fulani alikwambia hautaweza kufanya jambo fulani.

PUNGUZA WOGA ILI KUFANIKIWA.
Wapo pia baadhi ya wazazi mara nyingi huwajengea picha mbaya watoto zao na watoto hao kuamini kuwa hawewezi. Mfano mtoto wako kila wakati anafeli katika masomo yake, badala ya mzazi kumuonesha njia za kuweza kufaulu ila wewe unamkatisha tamaa. Mwisho wa siku mtoto huyo anajenga woga binafsi, na kuamini yeye hawezi.

Ndugu Msomaji wa makala hii, inawezekana hata wewe unashindwa kufanikiwa, hii ni kwa sababu kuna maneno ambayo uliambiwa na wazazi au ndugu wengine wanakuzunguka na leo hii bado unayakumbuka, mfano inawezekana uliambiwa wewe kichwa chako sio cha biashara na wewe ukayaamini maneno hayo.

Hivyo wakakwambia ujikite zaidi katika elimu yaani usome kwa bidii ili  uje kuwa mtu fulani hapo baadae.

Kwa kuwa uliamini kuwa huwezi kufanya biashara na ukajikita katika zaidi katika elimu. Umemaliza chuo, ajira hakuna kwa kuwa ulishaambiwa huna kichwa cha biashara leo hii unaona maisha yazidi kuwa magumu na huna njia nyingine za kujiongeza ili uweze kufanikiwa.

Huwa ni ukweli usiofichika wala hauhitaji mifano kutoka ulaya watu wengi tunashindwa kufanikiwa hii ni kutokana na woga binafsi tulionao. Wito wangu kwako ni kwamba ili uweze kufanikiwa unahitaji kujiamini, tumia akili, nguvu na kuwa na mawazo bora ya kufikiri yatakayokufanya wewe kutoka katika hali uliyonayo kusonga mbele kuyasaka Mafanikio. Naomba kwa Leo niishie hapo.

Usisite kumshirikisha mwenzako naye ajifunze kupitia mtandao huu wa DIRA YA MAFANIKIO kila wakati.

Imeandikwa; Benson chonya


dirayamafanikio@gmail.com

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.