google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Mar 15, 2016

Yasiyowezekena Ndio Mlango Wa Mafanikio Yako.

No comments :
Uhali gani mpenzi msomaji wa safu hii ya DIRA YA MAFANIKIO? Ni matumani yangu makubwa unazidi kuelimika kwa kujifunza mambo mbalimbali kupitia mtandao huu,  pia nakusihi  kila utakochojifunza kupitia mtandao huu ni vyema ukawashirikisha na watu wengine ili na wao waelimike zaidi. Kama ilivyo ada yangu kuweza kukumbusha baadhi ya mambo ambayo yatukufanya uzidi kusonga mbele kimafanikio kwa kila jambo unalolifanya ili kuweza kutimiza ndoto zako.
Katika makala ya leo tutakwenda kujikita zaidi kwa kutazama yale mambo ambayo tunayaangalia kwa jicho la kawaida na kuyaona mambo hayo kwamba hayawezekani. Lakini katika makala ya leo nakusihi ya kwamba kwa kila jambo ambalo unaona haliwekani jaribu kulitazama jambo kwa jicho la tofauti, endapo utayatazama mambo ya kimafanikio kwa jicho la tofauti hakuna jambo ambalo halitawezekana.
Kimsingi tulio wengi hatuamini katika kushinda ila tunaamini katika kushindwa, kuna usemi mmoja huwa unatumika katika michezo mbalimbali  unasema ya kwamba ‘’asiyekubali kushindwa siyo mshindani’’ vilevile hata katika safari ya mafanikio usemi huu unahusika sana kwa sababu kuna baadhi ya watu hawapo katika upande wa kuamini ya kwamba siku moja watakuwa zaidi ya Dongote au matajiri wengineo, swali la kujiuliza ni kwamba hao matajiri wa leo,  kama na wao wasingekuwa  fikra chanya za kuwa matajiri zaidi ya matajiri walikuwepo kwa kipindi hicho unafikiri leo hii wangekuwa hapo walipo leo hii?

Soma; Usipojiandaa Kwa Mabadiliko Haya, Hakuna Wa Kukusaidia Katika Maisha Yako.
Jambo jingine la msingi ni kwamba kama wewe ni mwanafunzi mara nyingi umekuwa unafeli hasa  katika masomo yako hasa somo la hesabu , unafikiri kufaulu somo hilo inawezekani au haiwezekani? Mwalimu wangu mmoja wa saikolojia  aliwahi kutufundisha kuhusu mafanikio alituambia ya kwamba katika safari yeyote ya mafanikio kila kitu kinawezekana,  baada ya kusema hivyo nilibaki nimeduwaa huku nikijiuliza anamanisha nini? Huku nikiendelea  kujiuliza,  akasema   ‘’ vitu ambavyo haviwezekani ni kumuomba dereva wa bodaboda  akupe tiketi au kumeza plasta huku ukitarajia ikutibu kitonda kilichopo nje ya mwili’’.  Hivo amini ya kwamba wewe kufaulu kimasomo inawezekana endapo utaweka nia za kweli.

KILA KITU KINAWEZEKANA KWAKO
Baada ya kipindi nilirudi nyumbani na kuwaza  ni kweli katika mafanikio kila kitu kinawezekana?  Nikaona jibu ni ndio kila kitu kinawezekana.  Nikajaribu kumuangalia mwanafunzi aliyehitimu kidato cha nne ambaye amefeli masomo yake. Wapo wengi hukata tamaa na kuamini maisha yao yameisha pale huku wakiwa wanaamini ya kuwa elimu ndio ufunguo wa maisha. Swali dogo la kujiuliza ni kwamba hawa waliofeli ina maana ya kwamba elimu imeishindwa kufungua maisha yao? Jibu ni kwamba sio kweli, ila  kufeli darasani sio kufeli maisha, jaribu kuangalia ni sehemu gani unaweza ukafanya vizuri na ukawa mshindi pia.

Soma; Umuhimu Wa Mahusiano Bora Katika Mafanikio.
Wapo baadhi ya wanafunzi wanaosoma vyuo akili zao zote wanazielekeza katika msingi ya kuajiliwa peke yake. Wanafunzi hao hawaamini katika misingi ya kujiajiri  wenyewe  pia na wao kuwajiri wengine. Katika hili nimebaini ya kwamba wanafunzi wengi ni wavivu wa kufikiri wao wanaamini ya kwamba kama mtu amesomea ualimu basi atakuwa mwalimu mpaka azeeke,  endapo  utakuwa na dhana hii mafanikio kwa upande wako yatakuwa magumu sana. Pia naomba nieleweka vizuri sio kuajiriwa ni kubaya la hasha bali jaribu kuwa na vyanzo vingi vya mapato licha ya kutegemea kuajiliwa  peke yake .
Vilevile kuna baadhi za jamii ambazo ni za wakulima na wafugaji wao wanaishi katika misingi ya imani potofu katika shughuli zao, hivyo kuwapelekea hata kushidwa kuzalisha bidhaa kwa wingi huku kufanya hivo wanaamini ya kuwa watalogwa. Kama wewe ni miongoni mwa watu wenye imani kama hizi jaribu kuachana na imani hizo mara moja na ufanya kazi kwa bidii kwa malengo ili kutimiza ndoto zako. Wewe ni miongoni mwa watu ambao wanauwezo mkubwa wa kuleta mabadiliko ya maisha yako na ya watu wengine  kwa sabaubu unaziona fursa nyingi za kufanikiwa hivyo usiwe kama samaki mwenye kiu ndani ya maji.
Mwandishi; Benson chonya
Simu; 0757-909942
E-mail; bensonchonya23@gmail.com

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.