Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Thursday, March 3, 2016

Faida Za Kujua Kile Unachokitaka Katika Maisha Yako.

No comments :
Kimsingi kila  mwanadamu anapenda kuwa na maisha mazuri siku zote,  hakuna hata mmoja ambaye anapenda kuishi katika maisha ambayo  sio mazuri hata siku moja. Baadhi wa watu hawa hasa ya wale ambao hawajafanikiwa  ukiwauliza kile ambacho wanakihitaji, wengi wao hutoa majibu ya ujumla kwamba nataka kuwa mfanyabiashara, nataka kusoma , nataka kujenga nyumba na vitu vingine vingi ambavyo mwanadamu huyu anataka kuwa  au kuvifanya kwa hapo baadae.
Lakini ukweli ni kwamba kusema hayo huwa tunakosea kwa sababu huwa tunayoongelea kwa mapana sana, hapa namaanisha ya kwamba lengo lako la kesho lazima liwe maalaumu. Kwa mfano usiseme unataka kuwa mbanyabishara na kuishia hapo tu, bali ni lazima uainishe ni aina gani ya biahara unayotaka kuja kuifanya na utie nia ya kweli juu ya biashara hiyo.
 Kwa mfano unaweza kupanga malengo yako ya hapo baadae unataka kuwa mfanyabiashara wa viatu, nguo za kiume, kike au viatu. Hata kama unataka kujenga nyumba katika maono yako lazima ufikirie  unataka nyumba ya aina gani? Iwe na vyumba vingapi, aina gani ya madirisha unatamani yawe kwenye nyumba yako na vitu vingine vingi.
Hizi ndizo faida ya kujua kile unachokihitaji kwenye maisha yako.
1. Huongeza kujiamini.
Baada ya kujua ni nini ambacho unachohitaji katika maisha yako. Itakusaidia sana kuweza kujiamini kwa kuweka jitihada za dhati za kufikiri na za kiutendaji katika jambo hilo. Mfano wewe ni mwanafunzi umejua ni nini ambacho unakihitaji katika masomo yako. Ni matumaini yangu makubwa utajenga uwezo mkubwa wa kujiamini na kufanya vizuri katika masomo yako ili aweze kutimiza ndoto zako halikadhalika wafanyabiashara na watu wengineo. Kujiamini ni siri kubwa kwa mtu yeyote msaka maendeleo. Baada  kujua ni nini ambacho unakitaka kutakusaidia sana   kuweka mikakati na mipango ili kutimiza lengo.

UKIJUA UNACHOTAKA, UTAHAMASIKA KUTENDA.
2. Kutokupoteza muda kwa mambo ambayo hayana msaada.
Mtu akijua anachokitaka mara nyingi huwa ni mtu ambaye anajali sana muda katika kutekeleza mambo yake. Vitu  ambavyo kwake havina faida kwake huachana navyo.  Kama mpaka dakika hii unatumia nguvu nyingi kwa kitu ambacho hakina manufaa kwako jaribu kukiacha kitu hicho na anza kufanya vitu ambavyo vitakuwa na manufaa makubwa kwako. Kwenye vitu ambavyo ni kweli unavitaka jaribu kuwa makini katika matumizi sahihi ya muda ili kuweza kupata matokeo mazuri  juu ya jambo hilo.
Mara kwa mara mtu ambaye anafanya vitu ambavyo anavipenda huangalia zaidi katika masuala yatakayomletea faida tu. Ila mawazo na mitazamo ambayo haina faida huachana nayo.
3. Huleta hamasa kubwa ya kiutendaji.
Ukifanya kitu unachokipenda mara nyingi huleta matokeo makubwa sana. Mfano wanafunzi wengi hawafanyi vizuri kimasomo kwa sababu wanasoma vitu ambavyo siyo chaguo lao. Mtu anapenda kusoma masomo ya biashara lakini wanampangia akasome sayansi, matokeo yake mtu huyu akifeli tunaanza kumlaumu kwamba  hana akili kumbe tatizo ni kumchagulia vitu asivyovitaka.
Halikadhalika hata wafanyabiashara walio wengi,  biashara zao zinakufa hii ni kutokana wanafanya biashara ambazo sio chaguo lao sahihi mwisho wa siku biashara hizo huzidumu. Moja ya kutaka kuona mafanikio ya kibiashara, elimu na vitu vingine hakikisha ya kwamba unafanya vile ambavyo kweli unavipenda kutoka moyoni mwako.
Kwa kuwa mafanikio yapo mikononi mwako, fikiri kwa makini mambo ambayo unahisi ni chaguo lako sahihi, na ukiyafanya kwa umakini wa hali ya juu utafanikiwa. Daima kumbuka usemi huu wa ushindi siku zote ‘my wish is my command.’
Asante sana kwa kuendelea kufuatila makala kutoka katika mtandao huu wa DIRA YA MAFANIKIO, ombi langu kwako washirikishe wenzako kadri uwezavyo ili wajifunze zaidi.
Makala hii imeandikwa na mtaalamu wa mipango na maendeleo Benson chonya.
Simu; 0757-909942
E-mail; bensonchonya23@gmail.com
Blog; dirayamafanikio.blogspot.com

No comments :

Post a Comment