Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Friday, March 25, 2016

Hizi Ndizo Fikra Chanya Za Kukusaidia Kufanikiwa.

No comments :
Mafanikio siku zote mbali na kufanya kazi kwa bidii yanahitaji uwe na fikra au imani chanya ili uweze kufanikiwa. Kwa kuendelea kuwa na fikra au imani sahihi inakupelekea kufikia mafanikio makubwa. Baadhi ya imani unazotakiwa kuwa nazo ili kujijengea mafanikio ni kama hizi zifuatazo:-
1. Amini kwamba pamoja na kushindwa kwako sana lakini una uwezo mkubwa wa kufanikiwa lakini ikiwa utajaribu tena na tena kile unachokitaka kwenye maisha yako.
2. Amini kwamba unatakiwa kufanya mambo yako kwa utofauti kama unataka kufika hatua fulani kimaisha. Acha kuishi kimazoea sana utakwama.
3. Amini ndani yako unao uwezo wa kufanya kitu chochote cha kukupa mafanikio ikiwa lakini utaamua iwe hivyo. Ukichukua hatua hali yoyote utaibadilisha.
4. Amini kufanya kazi kwa bidii ni njia pekee ya kukutoa kwenye umaskini. Kama unafikri natania angalia watu wengi ambao wanafanya kazi sana lakini huku wakikubali kujifunza. Maisha yao ni ya mafanikio makubwa.
5. Amini muda ulionao ndio unaouwezo wa kukufanya ukawa maskini au tajiri. Itatokea hivyo kwako kwa kupanga matumizi mazuri ya muda wako.

KUWA NA MAWAZO CHANYA.
6. Amini kuwa mbali na watu hasi ni njia mojawapo ya kukusaidia kufikia malengo yako.
7. Amini kwamba wewe ndiye unayeyajibika kwa maisha yako. Kwa vyovyote vile maisha yako yalivyo wewe ndiyo chanzo kikubwa cha kwanza hakuna wa kumlaumu.
8. Amini kuwa mshindani mkubwa wa kwanza wa maisha yako ni wewe. Unatakiwa kuwa bora kuliko jana kila siku.
9. Amini una uwezo mkubwa wa kujifunza kitu chochote na ukaweza. Unaweza kujifunza mafanikio, biashara au chochote kile unachokitaka.
10. Amini una uhuru wa kuchagua maisha yako yawe vipi. Kama unataka maisha yako yawe ya mafanikio makubwa huo ni uchaguzi wako au kama unataka maisha yako yawe ya kawaida pia huo ni uamuzi wako.
Ansante kwa kujifunza na endelea kutembelea DIRA YA MAFANIKIO kwa kujifunza zaidi.
Ni wako rafiki,
Imani Ngwangwalu,

Simu; 0713 04 80 35,
E-mail; dirayamafanikio@gmail.com

No comments :

Post a Comment