Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Monday, March 21, 2016

Mambo (5) Ya Kuyatazama Ili Kuongeza Thamani Katika Biashara.

No comments :
Huenda ukawa anafanya biashara au unapenda kufanya biashara lakini yapo baadhi ya mambo ya msingi ya kuyatazama kabla  au wakati wa kufanya biashara. Tupo baadhi yetu tunashindwa kufikia malengo yetu hasa katika kuwaza au tunapofanya biashara. Leo katika makala haya nitakwenda kukueleza juu ya kujijengea misingi ili kukuza  na kuongeza uthamani wa biashara.
Biashara yoyote ile endapo itafanywa kwa misingi ambayo inafaa itakuwa na faida sana. Zipo baadhi ya biashara hazikui kwa sababu  ya kuzifanya biashara hizo miaka yote kwa staili moja. Kama kweli unataka kukuza biashara yako ni lazima utazame ni kwa jinsi gani unaweza kubadilisha mfumo wa kiutendaji ambao utakufanya uweze  kupata faida zaidi. Biashara hata kama itakuwa ndogo au kubwa kiasi gani endapo utaifanya kwa ubunifu na umakini wa hali ya juu utaongeza wateja zaidi.
Yafuatayo ndio mambo ya msingi ya kuongeza uthamani wa biashara ili kuongeza wateja zaidi;
1. ladha na  fasheni.
Kimsingi kuna baadhi ya watu huwa tunafanya biashara tu bila kuangalia vitu kama  vile ladha  au fasheni (mitindo inayokwenda na wakati) . Huenda ukawa haujanielewa ngoja nikupe mfano, kama wewe unafanya biashara angalia wateja wako wanakula au wanakunywa kwa sababu ya kukidhi mahitaji au kwa sababu wanaridhika na kile wanachokula au kunywa. Kama wewe unafanya biashara nyingine kama vile, nguo, viatu, magari, vitu vya ujenzi vitu vingine ni lazima uangalie vitu vinavyokwenda na wakati , kwani endapo utafanya hivyo ndivyo vitavyokufanya uongeze wateja. Tukumbuke ya kuwa kadri vitu vinavyokuwa vya fasheni ndivyo wateja wanavyozidi kuwa wengi.

Mambo (5) Ya Kuyatazama Ili Kuongeza Thamani  Katika Biashara.
WEKA LADHA NA FASHENI KWENYE BIASHARA YAKO.
2. Kipato cha wateja.
Katika kutazama ni vipi unaweza kuongeza uthamani wa biashara jambo la msingi ni kujua kipato cha wateja wako.  Kama eneo ambalo unaishi wateja wako wanaoishi ni watu wa kipato cha kawaida ni lazima ujue ya kuwa bidhaa na bei lazima vilingane na wateja wako mfano huwezi kwenda kuanzisha biashara ya super market kijijini. Pia tukumbuke ya kuwa kuna baadhi za bidhaa endapo bei zitakuwa chini ndio huwa zinawateja wengi zaidi, halikadhalika kama wateja wako ni watu wa kipato cha juu basi bidhaa na bei ya bidhaa zako ni lazima yakidhi mahitaji ya watu hao kwa namna moja au nyingine.
3. Uhitaji wa bidhaa.
Katika biashara ni lazima uangalie uhitaji wa bidhaa au huduma kwa wateja wako. Kanuni za kibiashara zinasema kwamba kama bidhaa  zina gharama ndogo za uuzaji na uhitaji wa wateja hua mkubwa sana na kinyume chake inawezekana pia. Pia ni lazima usome soko lako kwa maana ya kuangalia wateja wako wanahitaji nini, na ujalibu kuchua mahitaji yao na kuwahudumia bidhaa hizo ili kukidhi mahitaji yao.
4. Matangazo.
Matangazo kuhusiana na jinsi ya upatikanaji na matumizi ya bidhaa au huduma husika. Ili kuwavutia wateja juu ya biashara yako ni vyema kuitangaza bidhaa yako ili kuwafanya  wateja waweze kuitambua biashara ambayo unaifanya. Katika kuitambulisha bidhaa katika matangazo ni lazima uwe mbunifu ili tangazo linapomfikia mtumiaji ahisi yeye ni sahemu ya biashara hiyo kwa maana ya kwamba mtumiaji aseme bila bidhaa hawezi kuishi.
5. Hali ya hewa.
Biashara yeyote ni lazima ujue ni kipindi gani bidhaa yako itauzika zaidi. Biashara zingine ni za msimu kwa mfano kama unauza miamvuli najua utaifanya kwa nguvu zaidi kipindi cha mvua. Hivyo kwa kuwa wewe ndo unataka kuifanya biashara au umekwisha kuanza biashara ni lazima uzingatie je biashara yako  itauzika zaidi msimu gani? Ukizingatia hayo, biashara yako itakuwa ni yenye faida kubwa sana.
Kama unataka kufanya biashara au unafanya biashara na unataka kupata faida kubwa ni lazima uzingatie hayo kwa namna moja ama nyingine.
Tunakutakia mafanikio mema katika biashara yako. Pia endelea kuwashirikisha wengine waweze kujifunza kupitia DIRA YAMAFANIKIO kwa kupata maarifa bora zaidi.
Makala  hii imeandikwa na Afisa mipango na maendeleo Benson Chonya
Simu; 0757-909942


No comments :

Post a Comment