google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Mar 7, 2016

Hiki Ndicho Chanzo Kikubwa Cha Kushindwa Kwako Katika Jambo Unalolifanya.

No comments :
Siku zote katika safari ya mafanikio, elewa ukweli huu kwamba hakuna tatizo lililo kubwa ambalo linauwezo wa kukuzuia kufikia mafanikio  yako unayoyataka. Hakuna rafiki atakayekuzuia kwenye mafanikio. Hakuna uchumi mbovu utakaoweza kukuzuia kufanikiwa. Hakuna hali mbaya yoyote kama kukosa wateja na hali nyinginezo eti ndiyo ikawa sababu ya kukuzuia kufanikiwa.
Chochote kile ambacho unaona ndiyo inaweza ikawa chanzo cha kushindwa kwako, tambua siyo kweli. Mara nyingi huwa kipo kitu kimoja tu ambacho wengi hawakijui na ndicho kinapelekea wewe ushindwe kwenye mambo yako mengi. Kitu hicho si kingine bali ni wewe mwenyewe. Wewe ndiye chanzo kikubwa cha kushindwa kwako.
Unaweza ukaona mambo mengine yaliyo nje yako ndiyo yanakuzui sana kufanikiwa lakini kama nilivyoanza na kusema sio kweli. Wewe ndiye mtu pekee unajizuia kwa sehemu kubwa kwenye mafanikio. Mambo mengine unayoyaona kama vile kuzuizi ni kweli yapo lakini hayo yana mchango kwa asilimia ndogo sana za kukuzuia kufanikiwa.
Najua unajiuliza maswali mengi sana kivipi? Sikiliza. Unajizuia kufikia kwenye mafanikio yako kwenye mambo mengi unayoyafanya wewe. Kwa mfano unajizuia kufikia mafanikio yako  hasa pale unapokata tamaa. Unajizuia kufikia kwenye mafanikio yako pia pale unaposhindwa kuamini kwamba utafanikiwa. Wakati mwingine unajizuia kwenye mafanikio yako kwa kushindwa kwako kuchukua maamuzi ya kukufanikisha.

Hiki Ndicho Chanzo Kikubwa Cha Kushindwa Kwako Katika Jambo Unalolifanya.
WEWE NDIYE CHANZO CHA KILA KITU.
Ukiangalia kwa kina utagungua chanzo kikubwa cha kushindwa kwako kinaanza na wewe. Kumbuka hauwezi kushindwa katika jambo lolote katika maisha yako mpaka wewe mwenyewe uruhusu hali hiyo ya kushindwa itokee ndani yako. Jaribu kufikiria katika maisha yako, jambo lolote lile ulilolishindwa , hukushindwa hivi hivi tu kwanza ulianza kukubali kutoka ndani yako kwamba sasa hapa siwezi tena kufanikiwa katika hili. Na kweli ilikuwa hivyo.
Kama hujaelewa vizuri ninachokwambia hapa nitakupa mfano. Naamini umewahi kupita shule na kuna wakati ulisoma somo la hesabu. Kama ulikuwa ukifanya vizuri, hongera. Lakini kama ulikuwa ukishindwa kila mara somo hili unajua ni kitu gani kilichokuwa kikitokea? Ni kwa sababu ulikuwa umeruhusu hali hiyo ya kushindwa hesabu iwe kwako. Na uliruhusu hivi kwa sababu ya zile sifa ambazo kila mtu anasema kwamba hesabu ni ngumu, basi na wewe ukajikuta unakubaliana na hali hiyo na kusema hesabu ngumu ukakubali kwamba utashindwa na ukashindwa kweli.
Kwa mantiki hiyo unaona kabisa hata katika mambo mengine ya kimaisha wengi wetu wanashindwa kufanikiwa kwa sababu ya wao wenyewe na si vinginevyo.  Unaweza ukasingizia sana hali yoyote kama wazazi wangu  hawakunisomesha au mimi sina mtaji na pia nimezaliwa familia maskini, yote sawa. Lakini kikubwa kumbuka wewe una mchango mkubwa wa kubadili maisha yako kwa zaidi asilimia themanini.
Unalo jukumu la kujikumbusha kila siku kwamba wewe ndiye unayewajibika kwenye maisha yako kwa kila kitu. Hivyo hutakiwi kukata tamaa, hutakiwi kujirudisha nyuma kwa mitazamo yako. Pia hutakiwi kujirudisha nyuma kwa kuwanyooshea wengine vidole kwamba ndiyo wamekufikisha hapo. Hiyo haitakusaidia sana zaidi ya kuchukua hatua ya kubadilika na kuendelea mbele.
Ansante kwa kusoma makala haya. Tunakutakia siku njema na endelea kujifunza kupitia DIRA YA MAFANIKIO kila wakati. Pia endelea kuwashirikisha wengine waweze kujifunza kutokana na makala tunazotoa hapa.
Ni wako rafiki katika kusaka mafanikio ya kweli,
Imani Ngwangwalu,
Simu; 0713 048035,

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.