google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Sep 25, 2017

Ubora Wako Unatokana Sana Kufanya Hivi…

No comments :
Kwa jinsi unavyofanya kitu chochote kile kwenye maisha yako, ndivyo unavyozidi kuwa bora zaidi katika kitu hicho.
Kwa mfano, kama wewe ni mwimbaji kwa jinsi unavyoimba kila siku na kufanyia mazoezi ndivyo unavyozidi kuwa bora katika uimbaji wako.
Kama wewe ni mwandishi, kwa jinsi unavyoandika kila siku, hivyo ndivyo unavyozidi kuwa bora katika uandishi wako.
Kama wewe ni mtu wa kujifunza vitu, kwa jinsi unavyojifunza, utashangaa unajikuta unakuwa ‘mlevi’ wa kutupwa wa kujifunza.
Kama wewe ni mtu wa kulalamika, kwa jinsi unavyoendelea kulalamika, hivyo ndivyo sasa utakuwa mlalamikaji mbobebezi, utalalamikia kila kitu.

Fanya kitu, uongeze ufanisi wako.
Kama wewe ni mtu mwenye tabia za kukopa kopa pesa kwa watu, utashangaa kwa jinsi siku zinavyokwenda unakuwa mkopaji kweli na una madeni kibao.
Kama wewe ni mtu wa kutoa sababu, basi hutafanya kitu cha maana, ni rahisi kuendelea kutoa sababu sana karibu kwa kila mtu.
Kama wewe ni mtu wa visasi, kuwa makini hapo, unaweza ukawa na mtu wa visasi kwa watu wengi sana kwa sababu ndio kitu unachokifanya.
Kama wewe ni mtu unayehakikisha jambo unalolianza lazima lifanikiwe, basi elewa utaendelea kufanikisha pia mambo mengine kwenye maisha yako.
Kwa chochote unachokifanya, bila kujali kitu hicho ni chanya au hasi utazidi kupta matokeo bora ynayoendana na kitu hicho unachokifanya kila siku.
Hebu jaribu kuangalia katika maisha yako ni kitu gani ambacho unakifanya sana? kwa kifanya kitu hicho utapata matokeo yake.
Hivyo basi kila wakati, chagua kufanya kwenye maisha yako mambo bora na fanya kila siku, baada ya muda utakuwa bora kwenye mambo hayo na kufanikiwa vikubwa.
Ni vigumu sana kuwa mshindi katika maisha yako kwa kufanya kitu mara moja na kutegemea mafanikio makubwa. Unatakiwa kufanya kila siku.
Kwa hiyo unaona mafanikio au kushindwa ni matokeo ya kufanya kitu fulani unachokifanya kila siku na kwa muda mrefu.
Kufanikiwa au kushindwa hakutokei mara moja kama wengi wanavofikiri, ni matokeo ya kuwekeza nguvu zako kila siku kwenye jambo hilo.
Anza leo kufanya mambo yatakayokusaidia kujenga ubora utakao kusaidia kufanikiwa sana na sio yatakayokuangusha.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,





No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.