google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Sep 8, 2017

Ijue Nguvu Na Siri Iliyopo Katika Matumizi Sahihi Ya ‘Diary.’

No comments :
Je unaifahamu ‘diary’, unayajua matumizi yake kwa usahihi?Nimeanza kwa kuuliza swali hilo ili tuweze kujua ukweli, maana watu wengi wanaijua ‘diary’ ila hawajui matumizi ya ‘diary’ hiyo. Wengi wetu huwa tunachanganya sana, wengi tumekuwa tukifanya matumizi ambayo yalitakiwa yafanyike kwenye notebook utakuta yanafanyika kwenye diary. Kama na wewe hujui nguvu iliyopo kwenye diary nakusihi twende sawa makala haya.
Kwanza kabisa naomba utambue ya kwamba kuna tofauti  kubwa kati ya diary na notebook. Na miongoni mwa kitu kikubwa ambacho hutafautisha vitu hivyo viwili ni; katika diary katika kurasa  kumeandikwa tarehe, mwezi pamoja na mwaka ila katika notebook hakujandikwa vitu hivyo. Tarehe, mwezi pamoja na mwaka ambavyo vimeandikwa katika diary  havijandikwa kama mapambo au havijandikwa kwa bahati mbaya ila vimeandikwa kwa sababu maalum.

Najua bado unashangaa, na unataka kujua nini nguvu na siri iliyojificha katika diary, wala usipate tabu ukweli upo hapa leo. Unajua walioitengeneza diary walikuwa na akili zao timamu, Waliitengeneza kwa kuweka mwaka, mwezi pamoja na tarehe ya siku husika, ili kukupa mwangaza wa namna ya kuitumia.
Na katika kuitengeneza vile walitaka diary ile iandikwe mambo ya msingi kwa kila siku, narudia tena walioitengeneza diary walitaka diary ile iandikwe mambo ya msingi kwa kila siku. Lakini lengo lao halikuwa sio kila kitu ni lazima kiandikwe katika diary. Najua unajiuliza ni mambo gani ya msingi ya kuandika katika diary?
Ipo hivi, kama ambavyo nilisema nilazima uandike mambo ya msingi katik diary yako kwa  kila siku na kwa tarehe husika , mwezi na mwaka husika, isitokee akaruka hata siku moja bila kuandika katika diary yako. Kwa mfano unaweza kuandika kila siku mambo ya msingi ambayo unataka kuyafanya kwa siku husika na siku hivyo ukafanya tathimini umetimiza jambo hilo kwa kiwango gani, kama umeshindwa kutimiza angalia ni wapi palipokufanya ushindwe kutimiza jambo hilo, majibu yote ambayo utayapata hakikisha unayaandika pia katika diary yako, kisha unaweka utaratibu wa kujikumbusha mara mara ili kupata ufumbuzi.
Kufanya matumizi ya aina hiyo katika diary yako, kutakusadia wewe katika kutimiza malengo yako. Lakini ikumbukwe ya kwamba  diary sio sehemu ya kuandikia notes ambazo haziusiani na mambo ya msingi yanayoihusu siku yako, bali diary ni kijitabu cha kuandika mambo yahusianayo na malengo ambayo unatakiwa kuyatimiza siku husika.
Hivyo kabla sijaweka nukta ni imani yangu umenielewa vyema, hivyo nakusihi uweze kuwa na diary yako na uweze kuandika kile ambacho nimekieleza hapo juu, kwani endapo hautafanya hivyo basi jiandae kubaki na maisha yale yale ya kila siku.
Ndimi afisa mipango: Benson Chonya

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.