google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Sep 9, 2017

Unaposhindwa Kwenye Jambo Lolote, Usikate Tamaa, Bali Endelea Hivi..

No comments :
Hakuna mtu ambaye anafanikiwa kwenye maisha yake moja kwa moja, bila kwanza kushindwa kwa namna moja au nyingine. Kushindwa kwa mtu ni kitu ambacho kinatokea karibu kwa kila mtu mwenye mafanikio. Inapotokea ukashindwa kwa chochote, usikate tamaa, endelea kuweka juhudi kubwa za kutafuta mafanikio yako. Mafanikio yote kabla hayajawahi mafanikio, yanaanza kwanza kwa kushindwa, hivyo kuwa king'ang'anizi mpaka kieleweke.

Unapoona umeshindwa kwa jambo fulani, usikate tamaa wala usihuzike, hilo ni fundisho kwamba unatakiwa kuweka juhudi na kutafuta njia mbadala ili kila ukitakacho kiweze kufanikiwa. Elewa unaposhindwa sio mwisho wa kufanikiwa kwako, maisha ya mafanikio zaidi ya hayo yanakuja na yanakusubiri wewe. Endelea kuweka juhudi na utambue kuna wakati mafanikio yako yanaanza kama kwa kushindwa.

Ni wako rafiki katika mafanikio,

Imani Ngwangwalu,
dirayamafanikio@gmail.com

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.