google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Sep 3, 2017

Sheria Za Lazima Kufuata Wakati Unatafuta Utajiri.

No comments :
Kama lengo lako katika maisha ni kutafuta mafanikio makubwa na hadi kufikia utajiri, zipo sheria za msingi ambazo unatakiwa kuzifuata na kufanyia kazi ili zikusaifdia kufika huko. Kwa kufuata sheria hizo zitakupa hamasa na mwongozo wa kufikia mfanikio yako unayoyahitaji kwenye maisha yako.
1. Wekeza kwenye maarifa.
Unatakiwa kuwekeza kwenye maarifa kila siku ili yakusaidie kutengeneza utajiri wako. Ukiwa tajiri, halafu ukakosa maarifa sahihi, utajiri huo kuporomoka itakuwa ni kitu rahisi sana. Unatakiwa kupata maarifa sahihi kila siku kwa kujisomea ili kulinda utajiri wako wa kesho, maarifa ni kitu cha muhimu sana kwako.
2. Fanya kazi sana.
Tumekuwa tukisema mara kwa mara, huwezi kufanikiwa sana kama unafanya kazi zako nusu, nusu. Unatakiwa ufanye kazi sana ili kufikia utajiri wako. Kazi ndio kitu pekee kitakachokufanikisha hata kama maisha yako yapo chini sana. Kama utatumia sheria hii ya kufanya kazi kuliko, haitakuangusha utafanikiwa lazima.

Kila wakati jiandae kwa chanagamoto za mafanikio.
3. Jiandae kwa changamoto.
Hakuna mafanikio utakayoyapata bila kukutana na chamgamoto. Kwa hiyo unatakiwa kila wakati kujiandaa na changamoto na uzishinde. Kama mafanikio yangekuwa ni rahisi basi kila mtu angekuwa nayo. Hivyo, unaona wengi wanashindwa kwa sababu ya changamoto hizi, ambazo wewe unatakiwa uzishinde.
4. Kataa madeni yasiyo na msaada.
Wakati unaelekea kwenye safari yako ya utajiri, kuwa makini sana na madeni ambayo siyo ya lazima kwako. Kama unakopa, kopa mkopo ambao moja kwa moja utauingiza kwenye biashara lakini sio kukopa kwa ajili ya matumizi ya kawaida. Unapokuwa upo kwenye madeni sana, unakuwa unajiingiza kwenye utumwa ambao sio wa lazima kwako.
5. Tengeneza picha kamili ya maisha yako unataka yaweje.
Hutakiwi kuishi tu kiholela, unatakiwa uwe na picha kamili ya maisha yako unataka yaweje baada ya kipindi fulani. Jinsi maisha yako unavyotaka yawe, unaweza kuandika kwenye karasi na kupitia karibu kila siku. Kwa kuishi kwa kanuni hii, itakusaidia sana kufikia utajiri wako kwa uhakika.
6. Tumia kile ukifanyacho kwa makini kukupa utajiri.
Chochote unachokifanya kina uwezo wa kukupa utajiri. Hakuna kazi maalumu ambayo unaweza ukasema kwa kuifanya kazi hiyo itakufanya lazima uwe tajiri. Kikubwa ishi kwa kujua kwamba kazi yoyote unayoifanya, ukiifanya kwa umakini mkubwa na kwa juhudi itakupa utajiri, hivyo acha visingizio chapa kazi.
7. Ishi maisha ya amani na watu wengine.
Hutakiwi kuwa mtu mkorofi kwa watu wengine, tengeza maisha ya amani kwa watu wengi. Hakikisha watu wengi wanafurahia sana uwepo wako. Hilo litakusaidia kupata watu wengi watakaokusaidia katika safari yako ya mafanikio. Ukitumia kanuni hii itakuwa na faida kwako sana wakati unaelekea kwenye utajiri.
Kwa kifupi, hizo ndizo sheria za msingi ambazo unatakiwa uzifuate ili zikusaidie kufikia mafanikio yako makubwa kila wakati.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.