google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Sep 23, 2017

Ongeza Uwezo Wako Wa Kufikia Mafanikio Yako Hivi…

No comments :
Haijalishi maisha yako ni mazuri  kiasi gani, lakini unayo nafasi ya kuyafanya maisha yako yakazidi kuwa bora kuliko ya hapo ulipo
Haijalishi una hali ngumu vipi za kimaisha, lakini unaweza kuboresha maisha yako kidogo kidogo na mpaka kuwa bora kabisa.
Haijalishi ni kwa jinsi gani unajua mambo mengi sana, lakini kwako ipo nafasi ya kujifunza na kuendeleza kupata maarifa yatakayokusaidia.
Chochote unachokifanya leo jiulize, kina uwezo wa kukua kesho na kuendelea kukupa mafanikio makubwa?

Ongeza uwezo wa mafanikio yako.
Ni kitu gani ambacho utakifanya leo na kikaendelea kukuweka juu tena na tena kwenye maisha yako ya kimafanikio?
Ukikaa na ukatulia, utagundua zipo njia ambazo zina uwezo wa kukufanya ukakua na kuongeza nafasi ya mafanikio yako sana.
Huhitaji kujilinganisha na wengine ili kuwa bora, unatakiwa kujilinganisha wewe tu mwenyewe na kuongeza ubora ulionao kila wakati.
Usikubali kuyafanya maisha yako yakaonekana mabovu kwa sababu ya kusimama au kuridhika kwa namna fulani.
Mashujaa katika maisha ni watu ambao wanajipa changamoto sana za kukua kila siku kwenye maisha yao.
Hicho ndicho kitu ambacho unatkiwa ujipe au ukifanye ili kufanikiwa. Unatakiwa ujipe changamoto ambazo zitakusaidia kukua.
Kwa mfano, kama umeamua kusoma, soma idadi kubwa sana ya vitabu ambayo itakufanya uwe mkomavu kiakili.
Kama umeamua kuwekeza, wekeza sana na isifike mahali ukatikisa kichwa na kusema kama ni kuwekeza sasa imetosha.
Unatakiwa kukua, unatakiwa kuongeza misuli ya kile ukifanyacho na kuwa kikubwa sna zaidi ya hapo ulipo kwa sasa.
Ukumbuke hakuna mtu ambaye ataweza kukuzuia katika hilo, zaidi yako wewe. Unao uwezo mkubwa wa kuongeza mafanikio yako.
Hautakiwi kusimama sasa, unachotakiwa kufanya sasa ni kuweka nguvu zako za uzingativu eneo unalotaka ukue.
Ukishaweka nguvu zako za uzingativu eneo hilo, anza kufanyia kazi huku ukiweka kila aina ya juhudi inayotakiwa ili kufanikiwa.
Nuia kubadilisha maisha yako tena, nuia kubadilisha matokeo ya maisha yako tena, nuia kubadilisha chochote maishani mwako.
Usikubali kukaa kama jiwe, mwanza wa mabadiliko katika maisha yako ni sasa kwa wewe kukubali kuuongeza uwezo wa mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,



No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.