google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Sep 1, 2017

Mafanikio Hayaendi Kwa Watu Hawa...

No comments :
Je, inafika wakati wakati katika maisha yako, wakati unang’ang’ana na kutimiza ndoto zako unajiona kama vile ndoto zako zinakuchanganya na kukukosesha raha?
Kama iko hivyo kwako, ni ishara tosha kabisa kwamba hutaki maisha yako yabaki hivyo, yaani kuna kitu ambacho unakitafuta na unataka kukibadili mara moja.
Mafanikio katika maisha hayaendi kwa watu walioridhika bali yanawafikia watu ambao kila wakijiangalia wanajiona hawana mafanikio kabisa.
Mafanikio yanakwenda kwa watu ambao hawalali, kila wakati wapo macho kuhakikisha ndoto zao zinatimia.
Mafanikio kamwe hayawezi kuwafikia watu ambao wanasema basi, hapo ndipo wamefika. Watu wa namna hii mafanikio yakiwafikia yanakuwa ya kitambo tu.
Kumbuka ili kufikia mafanikio makubwa hutakiwa kuridhika, ni kuendelea kujituma tena na tena, hapo utatengeneza mafanikio makubwa.

Ukiridhika kwa namna yoote ile, ujue kabisa utakuwa unatengeneza mazingira a kupishana na mafanikio yako wewe mwenyewe.

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.