google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Sep 16, 2017

Ili Ufanikiwe, Ishi Kwa Sababu Hii…

No comments :
Kipo kitu kwenye maisha yako ambacho kinakufanya uamke asubuhi na mapema. Kipo kitu ambacho kinakufanya uongeze juhudi zako hata kama unakutana na changamoto za kila aina. Kitu hicho kinaweza kuwa ni ndoto au yale malengo unayotaka kuyakamilisha kwenye maisha yako.
Hiyo yote inaonyesha unaamka asubuhi na unaweka juhudi bila kukata tamaa kwa sababu ipo sababu inayokufanya ufanye hivyo, sababu yenyewe si nyingine bali ni kukamilisha malengo yako. Hiyo hasa ndiyo sababu kubwa inayokufanya ufanye kila linawezekana mpaka kuona mipango yako yote inatimia.
Kwa hiyo unachotakiwa kuelewa ipo sababu, katika kila kitu ambacho unatakiwa kukifanya. Unatakiwa kuielewa sababu hiyo vizuri ili ikusaidie kuchochea moto mkubwa wa mafanikio ulio ndani mwako. Ukiwa huna sababu ya hicho unachokifanya utashindwa kuweka juhudi kubwa na mwisho wa siku utashindwa tu.

Ishi kwa sababu maalumu.
Anza leo kuishi kwa sababu, jiulize kitu hicho unachokifanya sasa, kwa nini unakifanya, chanzo cha msukumo wake ambao unatoka ndani mwake ni nini hasa? Ukishaijua hiyo sababu itakufanya usikate tamaa na kila wakati utatamani sana kukifanya kitu hicho ili utimize sababu ya kufanya kitu hicho.
Watu wengi katika maisha wanajikuta hawasogei sana au ni watu wanaotaka kusukumwa sukumwa tu, hiyo yote ni kwa sababu ni watu ambao hawajui hasa sababu ya kufanya hivyo wanavyotakiwa kufanya. Ukiwa hujui hasa sababu inayokusukuma kufanya jambo unalolifanya sio rahisi kufanikiwa.
Hata safari yoyote unapoianza asubuhi, sina shaka unakuwa una sababu kwa nini unaenda safari hiyo. Sijawahi kuona mtu anasafiri tu ilimradi asafiri, lazima awe na sababu huko anakoenda anaenda kufuata nini? Bila ya kuwa na sababu ya hiyo safari basi itakuwa safari hiyo ni kazi bure.
Halikadhalika, maisha yetu hasa kwa yale mambo tunayoyafanya yanatakiwa yawe na sababu haswaa, sababu ndio msingi wa kwanza wa kukusaidia kuweza kupiga hatua za kufanya hicho unachotakiwa kukifanya. Hatua zako zitakuwa imara na utafika mbali sana ikiwa unajua sababu ya kile hasa unachokifanya.
Chukua hatua leo na anza kuishi kwa sababu, hapo utafika mbali kimafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,









No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.