google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Sep 17, 2017

Sababu Zinazofanya Watu Wengi Kufanya Maamuzi Mabovu.

No comments :
Kati ya kitu kimojawapo kinachofanya watu washindwe sana kwenye maisha ya mafanikio ni kile kitendo cha kufanya maamuzi mabovu. Maamuzi mabovu yanaharibu na yanapoteza maisha ya mafanikio ya watu wengi sana.
Ni vyema kujua maamuzi mabovu ni chanzo cha kushindwa kwa watu wengi sana na maamuzi hayo mabovu yanafanywa karibu kila siku na wengi. Kitu cha kujiuliza, je, ni kwanini watu wengi wanafanya maamuzi mabovu ambayo yanapelekea kuharibu maisha yao?
1.  Mitazamo mibovu waliyonayo.
Kitu ambacho kinasemwa na wataalamu wengi wa mafanikio kwamba kinapelekea kwa watu wengi kuwa na mamuuzi mabovu mitazamo mibovu au ‘poor mindset’ walizonazo, hiki ndicho kitu kinachofanya watu wengi wanakuwa na maamuzi mabovu sana.
Hivyo ili kuwa na maamuzi sahihi, unatakiwa kuwa na mtazamo sahihi. Na mtazamo sahihi hauji hivi hivi tu bali ni matokeo ya kujifunza kila siku kupitia vitabu na kujua mawazo ya wengine. Ukijifunza hiyo ni njia itayokusaidia kuwa na mtazamo sahihi utakao kufanya uwe na maamuzi sahihi pia.

2. Kufuata sana maamuzi ya watu wengine.
Kuna wakati maamuzi mabovu yanakuja kwa sababu tu ya kufuata maamuzi na taratibu za jamii. Hapa unajikuta mtu unaamua jambo fulani kwa sababu jamii yako inafanya hivyo au inaishi hivyo na wewe unaamua kuamua  hivyo.
Mfano wa athari za maamuzi haya zinajitokeza kwa watu hasa wanapokuwa wanataka pengine kujiunga na masomo ya aina fulani, mathalani, utakuta kozi fulani inasemekana inalipa sana ukiisoma, kwa sababu hiyo utashangaa na mtu mwingine anaifuata, pengine kumbe kwa maamuzi hayo ni mabovu na kozi hiyo inaweza isimsaidie.
3. Kutokujielewa.
Mbali na maamuzi mabovu na kufuata maamuzi ya watu wengine kitu kingine kinachopelekea maamuzi mabovu ni kutokujielewa. Watu wengi wanachelewa sana kujielewa bila kujijua na matokeo yake hufanya maamuzi mabovu sana kila wakati.
Ili kuepuka kuendlea kufanya maamuzi mabovu elimu ya utambuzi inahitajika karibu kwa kila mtu ambayo itasaidia kufanya maamuzi yaliyobora. Bila kupata elimu ya utambuzi itakuwa ni kazi bure tu maamuzi mabovu yataendeea kufanikiwa na kuharibu maisha.
Kama tulivyoeleza kila wakati unapoona maamuzi mabovu yamefanikiwa sehemu yoyote ujue kabisa sababu kubwa zinazochangia ni pamoja na kutokujielewa, mitazamo mibovu na kufuata mitazamo ya watu wengine.
Chukua hatua na endelea kutembelea dirayamafaniko.blogspot.com kujifunza kila siku..
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.