google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Sep 12, 2017

Hizi Ndizo Aina Kubwa Za Hofu Zinazotawala Kwenye Maisha Ya Watu Wengi.

No comments :
Kwenye maisha zipo hofu ambazo zinatawala maisha ya wanadamu wengi kama sio wote. Hakuna mtu ambaye hana hofu hizo, isipokuwa hofu hizo zinakuwa zinatofautiana kati ya mtu mmoja na mtu mwingine.  Wengine utakuta ni watu ambao wana hofu hizo nyingi zaidi na wengine wana hofu hizo chache.
Kupitia makala yetu hii ya leo, nataka tujifunze pamoja aina za hofu ambazo zinawasumbua watu wengi sana duniani. Kwa mujibu wa mwandishi nguli wa vitabu dunia, Napoleon Hill ameeleza hofu hizi ambazo karibu kila binadamu anazo dunia zipo hofu kubwa za aina sita.

1. Hofu ya kuogopa kifo.
Karibu kila mtu aliye duniani linapokuja swala la kifo limekuwa likitishia amani au hofu kubwa sana. Hii inasemekana ni hofu ya kwanza ambayo watu wengi wanayo. Wengi wanahofia sana hasa wanapokumbuka kuna kufa.
2. Hofu ya kuogopa umaskini.
Harakati nyingi za maisha ya watu wengi duniani zinatokana na watu kupigana kuupinga umaskini. Hii pia ni hofu ambayo binadamu anayo, hataki kabisa kuuona umaskini ukiwa donda ndugu kwenye maisha yake. Wengi wamekuwa wakiishi kwenye hofu hii sana.
3. Hofu ya kuogopa uzee.
Pia hofu hii inatawala kwa wengi hasa wanapokumbuka kwamba uzee unakuja. Kila mtu anatamani aishi maisha yake akiwa kijana siku zote lakini ni kitu ambacho hakiwezekana kutokana na sababu za kimaumbile inakulazimu kuzeeka.
4. Hofu ya kuogopa kukataliwa na mwenzi wako.
Binadamu pia wamekuwa ni waoga kukataliwa na wenzi wao hasa wale wanaowapenda kwa dhati kutoka mioyoni mwao. Aina hii ya hofu pia inawatesa wengi hasa lile kundi linalopendana kwa moyo mmoja.
5. Hofu ya kuogopa kuwa na afya mbovu.
Ugonjwa pia ni kitu ambacho kimekuwa kikimtishia sana binadamu. Kila binadamu anapenda afya yake iwe bora wakati wote. Kwa sababu hiyo, hii ni hofu ambayo kila mtu amekuwa karibu anayo isipokuwa zinatofautiana tu.
6. Hofu ya kuogopa kukosolewa.
Kila mtu napenda kile anachokisema kikubalike na wengine. Hakuna mtu ambaye anapenda akosolowe sana. Kwa hiyo kutokana na hilo hii ni mojawpao ya hofu inayowasumbua watu wengi duniani, nikiwa na maana wengi hawataki kukosolewa, ukitaka ugomvi mkosoe mtu, utaona.
Kama nilivyoanza kusema hofu hizi zinatofautiana kati ya mtu mmoja na mtu mwingine. Lakini hizo ndizo hofu kubwa zinazotawala maisha ya mwanadamu wakati wote.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio.
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.