google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Sep 10, 2017

Usijaribu Kuiambia Dunia Kitu Hiki...

No comments :
Usijaribu kuiambia dunia kwamba unaweza kufanya kitu fulani, badala ya kusema hivyo, wewe onyesha kwa vitendo kwamba unaweza kufanya, hicho ambacho unataka kukifanya. Kwa lugha nyingine, jifunze  kuonyesha uwezo wako kwa vitendo na si kwa maneno kwani maneno peke yake hayata kusaidia sana. Vitendo vyako ni bora sana kuliko maneno unayotaka kuyaongea kila wakati.

Watu wengi wanaoshindwa katika maisha wana tabia sana ya kutaka kujionyesha kwamba wao ni wababe wa dunia na wanaweza kila kitu na kujikuta wakipoteza muda wao mwingi kuwaeleza wengine kwamba wanaweza kufanya badala ya kuweka vitendo. Usiendelee kupoteza muda wako kwa watu kuwafafanuliwa uwezo wako, wewe piga kazi, acha kazi itazungumza yenyewe.

Usijisikie vibaya pale watu wanapotaka kukusoa na kukwambia huwezi na wewe unajijua unaweza, upo wakati utafika kazi zako ndio zitakazozungumza na kuwaacha wakiwa mdomo wazi. Acha kuwa mtu wa maneno hata kidogo, piga kazi, wapiga kazi wote ndio washindi kwenye hii dunia. Mengine yote unayotaka kuyafanya ya kutaka kujionyesha ni kujipotezea muda wako bure.

Utumie muda wako kuweka akili na nguvu zako kutafuta matokeo uyatakayo na si kwa ajili ya kuwafurahisha wengine, hawatakusaidia kitu hao. Unaweza ukawa ni miongoni mwa washindi wakubwa katika safari ya mafanikio kama utaamua iwe hivyo wewe kuacha kufanya kazi kwa maneno na kufanya kazi kwa vitendo.

Naamini hilo kwako linawezekana na ushindi mkubwa wa mafanikio unakusubiri ukichukua hatua sahihi.

Ni wako rafiki katika mafanikio,

Imani Ngwangwalu,
dirayamafanikio@gmail.com

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.