google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Sep 13, 2017

Ikiwa Utajua Hatma Ya Maisha Yako Iko Hivi…Utafanya Nini?

No comments :
Ikiwa leo utajua kwamba utasababisha matokeo ya aina fulani kwenye maisha yako kama tu utafikiri kwa makini, utachukua hatua sahihi, utaweka nguvu za uzingativu siku hadi siku na hatua kwa hatua, ni kitu gani utakachofanya cha ziada, hebu fikiri?
Ikiwa tena leo utajua kama utaondoa kila aina ya shaka ndani mwako hiyo itakusaidia kutimiza malengo yako mapema, unafikiri ni kitu gani utajitoa kukifanya kwa ukamilifu kabisa katika maisha yako na kuwa huna shaka nacho hadi ukifanikishe?
Ikiwa utajua imani yako na kufikiri kwako kwa namna fulani ndiko kunako umba maisha yako yawe kama hivyo yalivyo, je, unafikiri utachagua imani ipi na  kufikiri kwa namna gani ambako kutakusaidi kubadilisha maisha yako?

Fikiri vizuri hatma ya maisha yako.
Ikiwa utajua pia nidhamu binafsi ndio msingi wa kukutengenezea maisha ya mafanikio unayoyataka, je, unafikiri utajenga nidhamu ipi binafsi ambayo itakusaidia kujenga maisha ya mafanikio makubwa maishani mwako?
Ikiwa utajua juhudi endelevu, juhudi za kila siku, juhudi ambazo hazina kikomo zikiambatana na kujifunza haziwezi kukuacha salama mpaka zikuache ukiwa na mafanikio, je, unafikiri utaweka juhudi hizo kwa muda gani bila kuchoka?
Ikiwa utajua umebakiza siku chache sana za kuishi duniani, maisha utakayoishi, utaishi maisha ya aina gani, muda utakaokuwa ukiutumia utakuwa unatumia muda wako kwa namna gani, ilimradi tu kuhakikisha unatimiza ndoto zako kwa muda mfupi?
Ikiwa utajua fursa za mafanikio zipo kila mahali na ikiwa utajua namna ya kufikia mafanikio yako, je unafikiri ni kitu gani ambacho utafanya ili kuzitumia fursa hizo kwa uhakika mkubwa hadi kufanikiwa?
Kimsingi, ipo nguvu kubwa sana ya kutenda kwa ziada au kutenda hovyo kama utajua hatma ya maisha yako inaishia wapi? Hapo tu inategemea umejua nini kwenye akili yako. unachotakiwa kutambua kwanza je, unajua nini?
Mara nyingi wengi wanashindwa sana kwenye maisha yao au wanatenda hovyo kwa sababu ya kutokujua hatma za maisha yao zinaishia wapi. Lakini hata inapotokea ukajua, je, unatumia kujua huko kukusaidia kufanikiwa?
Kitu cha msingi unachotakiwa kuelewa ni kwamba, ikiwa utajua kile unachotakiwa kukifanya kwamba ni cha msingi na kinakupa mafanikio makubwa, ni kitu gani ambacho utakifanya cha ziada na kikakupa manufaa na mafanikio?
Acha kuwa miongoni mwa kundi la watu ambao wanachezea sana fursa za mafanikio ingawa wana kila kitu wanachokijiua. Kuwa miongoni mwa watu wachache ambao wanafaidi kwa kujua kwao mambo au vinginevyo unataka kuendelea kuteseka?
Maisha ya mafanikio yanakuja kutokana na kujua vitu na kisha vitu hivyo kuvifanyia kazi na sio kujua tu peke yake na kuviacha vitu hivo vikiwa hewani bila msaada wowote. Jilulize leo kujua kwako kuna kusaidaia?
Je, kwa sasa unakutumia kujua kwako yale mambo ya msingi kuweza kukusaidia kufanikiwa katika maisha yako? Ikiwa utajua leo, umebakiza mwaka mmoja ili ufe nini ambacho utafanya, juhudi zipi utaweka na mikakati ipi utaweka?
Anza leo kuishi kwa kutumia falsafa ya ikiwa utajua…itakusaidia sana kuweza kubadili maisha yako na kuwa ya tofauti. Je, uko tayari ikiwa utafanya hivi… maisha yako yakatakuwa vile?
Chukua hatua na kufanyia kazi mambo haya ya msingi uiyojifunza hapa, au je bado unasitasita kuchukua tena hatua?
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.