google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Sep 22, 2017

Sifa Moja Ya Muhimu Sana Katika Kukupa Mafanikio.

No comments :
Mafanikio yako yanakuja kutokana na wewe kuwa wa muhimu. Mafanikio yako ya kweli hayaji kwa sababu ya bahati nasibu wala hayaji kwa sababu ya kuwanyonya watu wengine sana, mafanikio yako ya kweli na ya kudumu yanakuja kwa sababu ya wewe kuwa wa muhimu katika maisha yako.
Kwa jinsi yoyote ile unavyotafuta mafanikio unatakiwa kuwa wa muhimu na kutoa thamani inayohitajika ili kufikia mafanikio yako. Hutakiwi kuwepo kuwepo tu kwenye maisha yako, unatakiwa uwe na machango wa kimafanikio kila siku iitwayo leo.
Jiulize kitu gani ambacho utakifanya sasa kitakuwa na mchango na umuhimu kwenye maisha yako? Jiulize tena ni juhudi gani kubwa ambazo unaendelea kuweka mwenye kazi na hata kwenye maisha yako kwa ujumla?

Kuwa mtu wa thamani utafanikiwa.
Ni rahisi kuweza kuiba na kufanya kitu chochote ambacho sio haki ili ujipatie mafanikio. Lakini ukumbuke kwa njia hizo sio rahisi kabisa kupata mafanikio ya kweli yatakayokufanya ung’are na uwe miongoni mwa watu waliofanikiwa.
Kupata mafanikio ya kweli kunaanza ndani mwako kwanza, kutokana na thamani unayoitoa, ambapo thamani hiyo ndiyo itakayo kufanya kila kona uwe wa muhimu na kupelekea kila mtu akikutamani uwe nae karibu kwake.
Kwa hiyo mpaka hapo unaona ili kufanikiwa, unahitaji kuwa wa tofauti, unahitaji kuwa wa thamani, unahitaji kuwa wa pekee ili kutengeneza thamani ambayo ukiipata ni lazima uweze kufanikiwa hata kama mazingira yanakataa.
Kama unatilia shaka hilo la umuhimu wako kwenye maisha ya wengine, ngoja tu nikwambie wewe ni wa pekee sana na mchango wako mkubwa unahitajika katika maisha ya wengine pia ili uweze kuyabadilisha.
Kama una umuhimu mkubwa hivyo kwa wengine, jifunze kuweka juhudi kubwa sana kila siku ili kutengeneza umuhimu na thamani yako zaidi. Umuhimu wako hauji kwa kukaa tu, umuhimu wako unakuja kutokana na kujituma na kuweka juhudi hadi kufanikiwa.
Anza kuwa wa muhimu leo kwa kubadilisha maisha ya wengine, kwa jinsi unavyobadilisha maisha ya wengine unazidi kuwa baraka kwa wengine , nawe pia maisha yako yanakuwa yanabadilika vivyo hivyo.
Ni kipi unachosubiri kuwa wa muhimu? Kuwa wa muhimu, ni sifa mojawapo kubwa sana ya kukupa mafanikio yako.  Anza sasa na chukua hatua katika kuelekea kufikia mafanikio yako makubwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,



No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.