google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Sep 6, 2017

Ijue falsafa Hii Ya Pesa, Jinsi Inavyowatofautisha Kati Ya Watu Maskini na Matajiri.

No comments :
Uliwahi kusikia ya kwamba pesa ina makelele? Kama hujawahi kusikia ngoja nikwambie kitu leo kuhusu pesa. Pesa hii ambayo unaifahamu ndiyo ambayo inatufanya wengi wetu tuweze kuisaka usiku na mchana, hii yote ikiwa ili mradi maisha yetu yaweze kuimarika kwa kiwango fulani.
Lakini licha ya kuipata fedha hiyo, wengi wetu fedha hiyo imekuwa si rafiki kwetu, hii ni kwa sababu moja kati ya sifa kubwa ya watu ambao hawana mafanikio ni kwamba wamekuwa na maisha ya kawaida, hii ni kwa sababu watu hao wamekuwa wanaifanyia kazi pesa, ila  pesa hiyo kwa upande wao imekuwa haiwafanyii kazi.
Na hali yote hutokea kwa sababu kubwa moja, wengi wamekuwa hawataki kuifanya pesa izalishe kwa wingi, wengi kila pesa ambayo wamekuwa wakiipata wamekuwa wakiifanya katika matumizi ambayo yanaifanya pesa hiyo ipotee bure. Hebu jaribu kutafakari ni pesa kiasi gani ambazo zimepita mikononi mwako, na je pesa hizo zimejizalisha kwa kiwango gani?

Ukiwa na falsafa sahihi ya pesa utafanikiwa.
Bila shaka majibu ya swali hilo utagundua ya kwamba ni pesa nyingi zimepita mikono mwako na hujawahi kufanyia kitu chochote cha maana. Hivyo kwa misingi hiyo utagundua ya kwamba wengi wetu tumekuwa ni watumwa wa fedha, hii ni kwa sababu pesa imekuwa ikitupelekesha hasa pale ambapo tunapoipata.
Na ndiyo maana hapo awali nilikuuliza uliwahi kusikia ya kwamba pesa ina makele? Maana yangu ilikuwa ni hii; ninaposema pesa ina makele nina maana ya kwamba, mara baada ya mtu kuipata pesa amekuwa hajui ni nini cha kufanya. Utakuta mtu akipata pesa kila kilichopo mbele yake anataka kukinunua, kwa misingi hiyo utagundua ya kwamba ni utumwa kiasi gani tulionao katika fedha.
Hivyo Ili uweze kufanikiwa kifedha, ipo falsafa ya mafanikio ambayo inatumika kuwaongoza watu na hadi kufikia mafanikio hayo makubwa sana ya kifedha. Falsafa hiyo ndiyo inayopelekea wengine wakawa na pesa na wengine wakawa hawana, wengine wakawa matajiri na wengine wakawa maskini.
Kwa mfano, falsafa kubwa ya watu wenye mafanikio hasa linapokuja suala la pesa, ukilinganisha na wale ambao hawajafanikiwa iko hivi; watu wenye mafanikio falsafa yao ipo kwenye kuwekeza kila aina ya pesa wanayoipata hata iwe ndogo vipi.  Na kile kiasi kidogo kinachobakia hukitumia katika katika matumizi ya kawaida, lakini mara baada ya kuwekeza.
Wakati watu ambao hawajafanikiwa nao pia falsafa yao ya pesa ni kutumia kila pesa wanayoipata na kiasi kidogo kinachobakia hicho ndio huanza kujaribu kuwekeza. Watu wasio na mafanikio, matumizi ndio kipaumbele cha kwanza kabisa kabla ya uwekezaji wowote ule.
Bila kujali shida zetu tulizonazo, changamoto mbalimbali, Ili kufanikiwa unatakiwa kujiwekea falsafa ya pesa kama wanavyofanya matajiri, ni lazima uanze kuwekeza kwanza hata kwa pesa kidogo, halafu matumizi yatafuata, kinyume cha hapo utakwama sana na utashindwa kufikia uhuru wa kipesa.
 Je, unavyofikiri kwa falsafa hizo mbili, je, hali ya maisha inaweza ikawa sawa kwa watu hao wawili kutokana na matumizi ya hizo falsafa? Najua majibu mpaka hapo unayo kwamba falsafa ipi ni sahihi. Kama utatumia falsafa ya pesa ya watu wasiofanikiwa, tambua utakuwa hivyo na ukitumia falsafa ya pesa ya watu wenye mafanikio, utafanikiwa pia.
Mwisho tuweke nukta kwa kusema ya kwamba ni vyema uifanye pesa ikufanyie kazi  kuliko  wewe kuifanya pesa kazi, kwani kufanya hivyo ni kuwa mtumwa.
Imeandikwa Kwa ushirikiano wa Imani Ngwangwalu & Benson chonya.


No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.