google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Sep 29, 2017

Maeneo Manne Ambayo Unatakiwa Kuwa Msikivu Sana Ili Kujenga Mafanikio Yako.

No comments :
Usikivu ni moja ya kitu muhimu sana katika safari yako ya mafanikio. Unapokuwa msikivu inakusaidia kujifunza mambo mengi sana tofauti na ambapo ungejifanya wewe ni mjuaji wa kila kitu hali ambayo ingekufanya ukose mengi.
Kitu cha kujiuliza ni watu wangapi ambao ni wasikivu, bila shaka ni watu wachache sana ambao wanajenga utulivu wa kusikiliza wengine wanasema nini au wao wenyewe ndani mwao wanasema nini hadi kuweza kufanikiwa.
Kwa kawaida tunapozungumzia usikivu, wengi wanajua ni usikivu wa kuwasikiliza tu watu wengine. Lakini jinsi ilivyo upo usiku wa aina nne ambao kila mtu anatakiwa kuwa nao makini ili kujenga mafanikio yake.

Jenga hali ya usikivu mkubwa ili kujifunza.
1. Usikivu kwa wengine.
Unatakiwa kujifunza kusikiliza wengine wanasema nini, nini maoni yao kwako bila kujali wanachokisema ni chanya au hasi. Kuna kitu cha msingi na cha kubadili maisha yako utakipata kama ni msikilizaji wa wengine kuliko ambavyo ungebaki wewe kama wewe ukawa unafuata yako bila kusikiliza mtu yeyote.
2. Usikivu kwako wewe mwenyewe.
Pia unatakiwa kujisikiliza mwenyewe na kuheshimu maoni yako. Pengine unajiuliza kivipi? Ndani yako kuna sauti ambayo huwa inasema na wewe. Sasa, kuwa makini kusikiliza sauti yako, maana hio ni muhimu sana kuliko hata sauti zinazotoka nje. Ukiwa msikivu kwako utapata uwezo wa kujenga pia mafanikio yako.
3. Usikivu kwa dunia.
Kwa jinsi tunavyoishi, dunia inatufundisha mambo mengi. Unapopata changamoto kuna vitu unajifunza na kwa namna hiyo unatakiwa kujua kujifunza jinsi dunia inavyosema na wewe. Utakuwa ni mtu wa ajabu kama hutaki kabisa kujifunza kutokana na dunia. Yapo mafundisho mengi sana unayoyapata  hata huhitaji kwenda shule.
4. Usikivu kupitia maarifa.
Vile vitu unavyojifunza vina sema bila kujali ni maandishi au kitabu. Sasa jifunze kusikiliza kile ambacho waandishi wanasema, kitabadilisha maisha yako kuliko jinsi ambavyo unang’ang’ana na kuwa mbishi bila kutaka kubadilika. Ukiweza kuyatumia maandishi vizuri yatakusaidia sana kuboresha maisha yako.
Hayo ndiyo maeneo muhimu ambayo unatakiwa kuwa msikivu sana ili yaweze kukusaidia kujenga mafanikio yako. Fanyia kazi maeneo hayo ili yawe msaada mkubwa kwako.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.