Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Friday, July 7, 2017

Fanya Mambo Haya Tu, Utakuwa Na Furaha Wakati Wote.

No comments :
Kati ya hitaji kubwa la  binadamu ambalo analihitaji kila siku ni kutafuta furaha ya kweli. Ukiangalia shughuli nyingi na vitu vingi ambavyo anakuwa anafanya binadamu, karibu vyote, vinakuwa vinalenga katika kupata furaha halisi na ya kweli.
Pamoja na kwamba furaha inatakiwa sana, lakini bado wapo watu ambao hawana furaha hiyo kabisa maishani mwao. Watu hawa wamekuwa ni watu wa kuishi maisha yanayowanyima furaha na wakati mwingine unaweza ukashangaa.
Sina shaka katika maisha yako umeshawahi kuwaona watu  ambao ukiwaangalia, unaweza ukawaona kama ni watu ambao wanafuraha karibu siku zote na pia wapo watu ambao ukiwaangalia unaona kama ni watu ambao hawana furaha.
Umeshawahi kujiuliza tena ni nini siri iliyopo kwa wale watu wenye furaha na kwa nini pia wale watu wengine hawana furaha? usihangaike sana kutafuta jibu, leo nataka nikupe siri yakutengeneza furaha kubwa ikiwa lakini utafanya mambo haya;
1. Samahe.
Dunia ina kero  na maudhi mengi sana.ikiwa utakuwa ni mtu wa kukasirika, unaweza ukakasirika mpaka upasuke. Siri ya kubaki wewe kama wewe na kujilinda na furaha yako ni kusamehe pale unapokosewa.
Ukishikilia mambo na kuweweka sana kifuani, hautaweza kuwa na furaha kamwe. Kuna mtu amekuuzi, msamehe na kisha endelea na maisha yako. Hautapungukiwa na kitu ukiamua kutoa msamaha wa bure, zaidi utajipa baraka.
Ishi sasa kwa furaha kubwa.
2. Ishi sasa.
Utajipoteza kwenye maisha ikiwa wewe ni wa kuishi jana au kesho sana. Siri ya kutengeneza furaha ya kudumu wakati wote pia ipo kwenye kuishi sasa. Acha kuchukua mambo ya jana au kesho ukaishi nayo leo, kwa kufanya hivyo utajibebesha mzigo mzito ambao utakufanya moja kwa moja ukupotezee furaha.
3. Acha kuchukulia mambo kwa ujumla.
Inapofika wakati mtu mwingine akakufanyia kitu ambacho hakieleweki na kumwona ndivyo kama alivyo, utakosea, acha kuchukulia mambo kwa ujumla.  Acha kuwaza kwa sababu fulani kasema hivi ndivyo ilivyo, au kwa sababu fulana kanifanyia hivi ndivyo ilivyo, fanya uchunguzi pata majibu ya jumla, kisha amua.
4. Elewa siku mbaya ipo.
Sisi binadamu tunakutana na mengi. Kuna wakati unaamka unajikuta yaani hujisikii kufanya kitu cochote na uko hovyohovyo. Hili linamtokea karibu kila mtu na sina shaka na hilo, kama siku hizo zipo, jiandae, ili usije ukapoteza furaha yako. ikitokea namna hiyo ujue jinsi ya kukabiliana na hilo.
5. Thubutu kufanya jambo jipya.
Watu waliofanikiwa kila wakati wanajaribu kufanya mambo mapya ya kuwapa mafanikio. Ni watu ambao hawachoki kujaribu mpaka kuhakikisha wanapata wakitakacho. Kwa kujaribu huko hujikuta wanapata uzoefu na kuondoa hofu na matokeo yake  wanajenga furaha ambayo inawasaidia kwenye maisha yao.
6. Chukua jukumu lote la maisha yako.
Ukiuelewa ukweli kwamba, maisha yao yanakuhusu wewe, hutakiwi kumlaumu mtu yoyote iwe serikali, mzazi au mwajiri wako basi utakuwa na furaha.kwa sababu kila kinachotokea utaona ni chako na kinakuhusu kwa asilimia zote utakuwa huna haja ya kulaumu mtu yoyote zaidi yako wewe.
7. Acha mambo mengine yaende.
Huna haja  ya kung’ang’ania hofu, huna haja ya kung’ang’ania kushindwa kwa jana wala huna haja ya kung’ang’ania mambo yale uliyoumizwa nayo na kuyaweka kwenye akili yako. Yaruhusu mambo hayo yaende,  jukumu lako ni  kujifunza, kuishi na kutabasamu ili kupata furaha ya kweli. Hayo mengine yote yameisha.
8. Kuwa mtu wa shukrani.
Kati ya kitu cha msingi sana katika maisha ni kujijengea utaratibu wa kuwa na shukrani. Kua mtu wa shukrani, kushukuru kile ulichonacho, kushukuru afya uliyonayo na kushukuru kila unachokipata. Ukifanya hivyo utataweza kuwa na furaha na hutapata shida hata ikitokea umekosa mambo mengine.
9. Jenga tabia ya kujiamini.
Amini kila wakati unaweza ukafanikiwa. Amini kla wakati una uwezo mkubwa ndani yako na pia waamini wengine kwa yale majukumu unayowapa. Ukiweza kujiamini wewe na hata kuwaamini na wengine, basi hautakuwa na wasiwasi katika maisha yako, kwa hali hiyo itukapa furaha.
10. Wasaidie wengine.
Unapokuwa msaada kwa wengine kwa kuwapa kile kitu ambacho unaona kuitawasaidia basi hio ni njia mojawapo ya kutengeneza furaha halisi na ya kudumu. Kuanzia leo anza kuwasaidia wengine kwa chochote ulichonacho. Fanya kile unachoweza na sio lazima iwe pesa., toa msaada wowote kwako na utajisikia vizuri.
Kwa kujua mambo hayo naamini yatakusaidia sana kuweza kukujengea furaha ya kweli ambayo itadumu maishani mwako. Kitu cha msingi kwako chukua hatua na utaona maisha yako yakibadilika.
Kila la kheri katika kufikia mafanikio  makubwa na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kujifunza kila siku.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Blog, dirayamafanikio.blogspot.com
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com

No comments :

Post a Comment