Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Thursday, July 13, 2017

Mambo Manne (4) Ya Kufanya Kila Siku Ili Kutengeneza Utajiri Endelevu.

No comments :
Kwa kawaida yapo mambo ya msingi sana ambayo kwa mtu yoyote mwenye nia ya kuwa tajiri lazima ayafanye mara kwa mara au kila siku ili kufikia utajiri huo. Pasipo kufanya mambo hayo hakuna kitu ambacho kinaweza kusimama na kuleta mafanikio.
Kwa wengi ambao hawayajui mambo hayo ndio hujikuta wakiishi maisha magumu karibu kila siku yasiyo na unafuu. Kwa kuwa DIRA YA MAFANIKIO haina choyo na wewe, leo tutajifunza pamoja mambo ya kufanya kila siku ili kutengeneza utajiri endelevu.
1. Toa visingizio vyote.
Kati ya jambo ambalo nimekuwa nilikilisema sana kwa mtu yeyote anayetafuta mafanikio ni kuachana na visingizio. Hilo liko wazi hivi, hauwezi kuwa tajiri kama wewe ni mtu wa visingizio kila siku, hapo elewa kabisa mafanikio kwako hayapo.
Sababu unazozitoa kwamba hujafanikisha jambo hili au lile, kweli ni nzuri, lakini haziwezi kukusaidia, kwani dunia haielewi sababu hizo zaidi ya kukutaka wewe  ulete matokeo ya mafanikio.
Hata kama ukiendelea kutoa sababu haitasaidia kitu, kikubwa, amua kutoa visingizio vyote na kama ni nguvu, tumia nguvu zako zote na kuhakikisha unaweza kufanikiwa kwa hicho unachokifanya na kujenga utajiri mkubwa kwenye maisha.

Jenga tabia ya kuwekeza maeneo mengi utafanikiwa.
2. Wekeza.
Jambo lingine mbali na kutoa visingizio unalotakiwa kulifanya maishani mwako na kutengeza utajiri ni kuwekeza. Inatakiwa kila wakati upime na kuangalia ni wapi uwekeze nini ambacho kitakua na manufaa.
Uelewe tu kwamba utajiri unajengwa kwa kuwekeza, utajiri haujengwi kwa mshahara mkubwa, utajiri haujengwi kwa njia za mkato mkato kama unavyofikiri, siri kubwa ya utajiri mwingi ni kuwekeza.
Ikiwa hujaanza kuwekeza kwa uhakika, anza leo kuwekeza chochote unachoona kinaweza kikakupa pesa kwa hapo baadae na kufanikiwa kujenga utajiri mkubwa. Ukifanya hivyo, maisha yako yatabadilika sana.
3. Piga hatua kila  siku.
Usikubali kusimama hapo ulipo hata siku moja, jitahidi sana kwenye maisha yako kupiga hatua kila siku. Piga hatua za kuelekea kwenye ndoto zako, yaani fanya kitu angalau kidogo ambacho kitakusogeza karibu kabisa na ndoto zako.
Unapofanya hivi siku hadi siku, utashangaa unasogea pasipo hata kujua. Maisha kwa jinsi alivyo yamekaa katika hali ya mwendo. Hivyo unatakiwa kuchukua hatua za kuelekea mbele bila kujali hatua hizo ni kidogo au kubwa.
Hata watu wenye mafanikio, karibu kila wakati ni watu wa kuchukua hatua, hufanya hiki na kile, ilimradi kuhakikisha wanasogea pale walipo. Ukifanyia kazi hili kila siku, uwe na uhakika hivyo ndivyo utakuwa unajenga utajiri wako.
4. Jenga matandao wa kimafanikio.
Mafanikio hayawezi kuja kwa kuyapata peke yako. Jitahidi sana kujenga mtandao wa kimafanikio ambao utakusaidia kila siku. Unapokuwa na mtandao huu inakuwa ni rahisi kupiga hatua kuliko ungekuwa huna.
Iko hivyo kwa sababu, utapata ushirikiano mkubwa, isitoshe mtandao wako huo kuna wakati utakupa habari za fursa kiasi cha kwamba hiyo pekee inakurahisishia wewe kujua maeneo ya kuwekeza ambayo hukuyajua.
Kwa kuhitimisha, huhitaji kujiuliza sana ufanye nini ili uwe tajiri, hebu kwa kuanzia fanya mambo hayo. Kama ukifanya mambo hayo kwa uhakika na usipokuwa na pesa ndani ya miaka mitano, basi naweza nikasema wewe ndio basi tena.
Nikutakie kila la kheri katika kufikia mafanikio makubwa na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kwa ajili ya kujifunza na kuhamasika kila siku.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,


No comments :

Post a Comment