google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Jul 14, 2017

Misingi Bora Ya Kufuata Ili Kujenga Afya Ya Mwili Wako.

No comments :
Katika maisha moja ya kitu cha msingi sana ambacho hutakiwi kukikosa ni afya bora. Kosa yote, lakini usikose afya bora, afya bora ina muunganiko na mambo mengi sana kwenye maisha yako ikiwa pamoja na mafanikio.
Naomba uelewe hivi, unapokuwa hauna afya nzuri, hakuna ambacho unaweza ukakifanikisha, utashindwa kwenye mambo mengi kwa sababu ya kushindwa kuweza kuyafanya kwa ufanisi kutokana na tatizo la afya yako.
Kwa mantiki hiyo,  mpaka hapo unaona ni kwa namna gani afya ilivyokuwa ya muhimu sana kwenye maisha yako. Sio suala la kuhoji tena ni lazima uwe na afya bora. Ni kwa namna gani utaweza kutengeneza afya bora?
Ifuatayo Ni Misingi Bora Ya Kufuata Ili Kujenga Afya Ya Mwili Wako.
 Msingi wa kwanza,  kunywa maji kwa wingi.
Maji mengi mwili yanasaidia mwili wako kuwa katika hali nzuri wakati wote na kusababisha baadhi ya viungo kufanya kazi kwa ufasaha. Hivyo, unalazimika kunywa maji kwa wingi kila wakati ili kuweza kulinda afya ya mwili wako ili iwe bora wakati wote, kinyume cha hapo itakuwa ni shida kwako.

Kunywa maji kwa wingi kila siku.
Msingi wa pili, soma kabla hujalala.
Unaposoma kitu kipya kabala hujalala unaifanya akili yake iende kupumzika huku ikiwa na wazo jipya au kitu cha kufanyia kazi usiku wote. Ukumbuke hapa mawazo yako ya kina yanafanya kazi muda wote kwa saa 24 . Soma kitu kipya chanya angalau nusu saa kabla hujalala kila siku itakusaidia sana.
Msingi wa tatu, fanya tahajudi (Meditation).
Tafuta eneo lilotulia na kila siku jitahidi kufanya tahajudi ama meditation. Hiki ni kipindi ambacho unatakiwa ukae kwa utulivu ukitafakari maisha yako na kutafakari kile unachokitaka katika maisha. Unaweza ukafanya tahajudi/meditation angalau hata kwa dakika 15 kila siku.
Msingi wanne,  fanya mazoezi.
Unatakiwa pia ujenge tabia ya kufanya mazoezi kila siku ili kuupa mwili wako afya. Fanya mazoezi ya kukimbia, fanya mazoezi ya kuruka au fanya mazoezi ya kunyanyua vitu vizito. Ukifanya mazoezi kila siku na ikawa ndio kitu endelevu mwili wako utakaa katika afya nzuri sana kila wakati.
Msingi wa tano, kula chakula bora.
Mwili wako haujengwi kwa matofali, mwili wako unajengwa kwa chakula safi. Kwa kulijua hili kila wakati jitahidi sana kuulisha mwili wako chakula ambacho kitakusaidia wewe kuweza kuujenga mwili wako kwa  afya bora. Tafuta vyakula safi vitakavyo ulinda mwili wako na magonjwa.
Kimsingi, afya yako haijengwi kwa kubahatisha. Afya inajengwa kwa kuzingatia msingi ya afya bora kama ilivyoainishwa katika makala haya ya leo. Usisubiri hadi uende kwa daktari, zingatia mambo haya nawe utakuwa na afya bora.
Endelea kujifunza kupitia dira ya mafanikio.blogspot.com kila siku kwa ajili ya kujifunza na kuhamasika.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Blog; dirayamafanikio.blogspot.com
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com


No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.