Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Sunday, July 30, 2017

Tabia Tano Muhimu Ambazo Ukizifuata Zitaboresha Maisha Yako Sana.

No comments :
Tabia ni msingi mkubwa sana wa mafanikio yako. Ukijenga tabia njema uwe na uhakika utafanikiwa na kufika mbali sana kimafanikio.
Leo nataka tuangalie kupitia makala haya, tabia ambazo ukizifuata na kuzitekeleza zitafanya maisha yako kuwa bora na  ya thamani kila iitwapo leo.

Tumia tabia bora za mafanikio zikufanikishe.
1. Usifanye kazi mbili kwa wakati mmoja.
Mawazo yako yote weka kwenye kitu kimoja unachokifanya. Ukiweka mawazo kwenye vitu viwili, utashindwa kuvifanikisha vyote kwa ufasaha na utashindwa.
2. Usigombane na mtu mpumbavu.
Kama kimetokea kitu cha kutoelewana na mtu ambaye unamwona hajielewi, achana naye ili asije akakupotezea muda wako bure.
3. Usiingie kwenye mabishano yasiyo ya lazima.
Fanya kile unachokiamini, kubishana kwingi na kujaribu kuonyeshana eti nani ni mshindi ni mambo ambayo yanapoteza muda wako pia. Epuka kubishana.
4. Usifanye maamuzi bila ya kufikiri sana.
Kama unataka kufanya maamuzi bora na ya maana kwako, yafanye kile kipindi ambacho akili yako imetulia, ukifanya maamuzi kwa haraka utajipoteza.
5. Usiende kulala ukiwa na hasira.
Unapolala huku una hasira, elewa kabisa hasira hizo utaamka nazo siku inayofuata, hivyo nenda kitandani ukiwa na amani itakusaidi sana.
Hizo ndizo tabia tano za msingi zenye uwezo wa kuboresha maisha yako ikiwa utaamua kuzifanyia kazi kwene maisha yako.
Kila la kheri katika kuboresha maisha yako na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kujifunza kila siku.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Blog, dirayamafanikio.blogspot.com
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com

No comments :

Post a Comment