Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Tuesday, July 18, 2017

MAFANIKIO TALK: Faida za Kushiriki Maonyesho Yoyote Yale Ya Kibiashara.

No comments :
Nikualike kwa mara nyingine tena katika kipindi hiki cha mafanikio talk ambacho kinakujia kila siku ya jumanne. Na siku ya leo tupo Patrick Kyando (star intergrated) kutoka Makambako. Licha ya kuzungumza    naye mambo mbalimbali ya kimafanikio , yeye yeye aliweza kutushirikisha faida za mfanyabiashara kushiriki katika maonesho.
Kwani wafanyabiashara wengi na wasio wafanyabiahara wamekuwa hawafahamu umuhimu wa kushiriki katika maonesho ya kibiashara ambayo yamekuwa yakifanyika ndani na nje ya Tanzania. Kama wewe ni miongoni mwa watu hao makala haya yanakuhusu, hivyo ni vyema twende sawa aya kwa aya.
Kuna  faida zaidi ya tatu kutangaza biashara ktk maonyesho yoyote :
1. Ukishiriki katika maonesho yeyote yale ya kibiashara  na ukiwa  na bidhaa ni rahisi kuuza kwa kuwa huwa kunakuwepo na watu tofauti toka sehemu tofauti ambao si rahisi sana kukutana nao ukiwa  kwenye kituo chako cha biashara. Hivyo ni muhimu kwako kuchangamkia fursa ya maonyesho kila yanapojitokeza ili kuweza kufaidika na faida hii.
2. Ukishiriki katika maonesho, ni fursa kwako kwa sababu unafungua ukurasa mpya kupata wateja wapya hata kupelekea kupata ‘network’ ya kibiashara, na ‘network’ hii huwa ni  endelevu kwa sababu utaweza kupata mawasiliano endelevu ya watu tofauti tofauti.
3. Utajifunza kutoka kwa wengine wanaozalisha au kuuza bidhaa kama zako kwasababu  wao wanakuwa na nafasi ya kuzielezea  kwa uwazi zaidi. 
4. Utajifunza vitu tofauti vya kibiashara na hasa mambo ya kiteknolojia ambayo wewe mwanzoni mwa biashara hiyo ulikuwa huijui.
5. Pia taasisi mbali mbali za serikari zinakuwepo kutoa elimu na huduma pia huwa  ni rahisi zaidi kuzipata eneo hilo la maonyesho kuliko wakiwa kwenye vituo vyao vya kazi.
6. Makampuni mengi hutangaza ofa  za maonyesho husika hivyo ni nafasi ya kupata bidhaa kwa bei  za ndogo zaidi.
Hivyo ni vyema na wasaa mzuri kwa wewe mfanyabiashara na usiye mfanyabiashara kuweza kushiriki  kwa namna moja ama nyingine katika maonyesho ya kibiashara  kwani kuna faida lukuki.
Kwa niaba ya uongozi wa mtandao huu wa dira ya mafanikio, nipende kumshukuru sana ndugu Patrick Kyando wa star intergrated kwa somo hilo zuri.
Mpaka kufikia hapo sina la ziada nikutakie siku njema na mafanikio mema. Tukutane jumanne ijayo katika kipindi hiki cha mafanikio talk. Kama unatamani siku ya jumanne ijayo tuweze kutupa somo kutoka kwako tuma neno mafaniko talk kwenda 0757 909 942 au tuma neno hilohilo kwenda e-mail yetu dirayamafaniko@gmail.com nasi tutakutafuta kwa ajili ya mahojiano mubashara.
Endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kwa ajili ya kujifunza na kuhamasika.
Habari njema, kama wewe ni mfugaji wa kuku, kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana na DM POULTRY FARM PROJECT, hawa ni wauzaji wa vifaranga vya kuku wa KIENYEJI ASILIA, SASSO NA KUROILER. Bei ya kifaranga kimoja ni Tsh 2000 pia kuna punguzo la bei kwa wateja watakaonunua vifaranga 500 na kuendelea. Pia tunatoa elimu ya ufugaji wa kisasa kwa wateja wa vifaranga. Hii elimu ni bure. Kwa mawasiliano zaidi tupigie simu namba 0767 04 80 35/ 0686 14 10 97. Tupo TANGA na vifaranga unatumiwa popote pale ulipo kama upo nje ya TANGA. 
Ndimi afisa mipango Benson Chonya,
bensonchonya23@gmail.com.

No comments :

Post a Comment