Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Sunday, July 16, 2017

Yafanye Maisha Yako Yawe Ya Mafanikio Kwa Kuanza Kuchukua Hatua Hii…

No comments :
Kama unakumbuka kupitia historia ujenzi wa piramidi kubwa za Misri, haukuanza kwa kujengwa na mawe mengi kwa pamoja, bali zilianza kujengwa kwa jiwe moja tu, tena jiwe hilo ambalo liliwekwa na mhudumu mmoja katika siku hiyo ya kwanza ya ujenzi.

Hilo jiwe moja liloanza kujenga piramidi hizo kubwa kihistoria na kupelekea mamilioni ya watu leo hii kutembelea Misri, lilionekana jiwe hilo ni la kawaida tu na wala halina chochote na wala mchango wake haukuweza kuonekana mara moja.

Hata yule mfanyakazi mtumwa ambaye aliweza kuweka lile jiwe la kwanza katika kujenga piramidi hizo hakuweza kutambuliwa wala kuonekana ana mchango wowote zaidi alizidi kuonekana ni mtumwa tu na asiye na maana yoyote.

Pamoja na kwamba umuhimu wa kujenga piramidi haukuonekana na mtu yeyote, na pia wala hakuna aliyejali ni nini kinaendelea, lakini kutokana na nguvu ya kuanza mwisho wa siku piramidi zilisimama na kushangaza watu wengi.


Kama nilivyotangulia kusema, leo mamilioni ya watu duniani wanasafiri tena kwa gharama kubwa kwenda kuangalia piramidi hizo za kihistoria ambazo ni matokeo ya kazi iliyoanzishwa na uwekaji wa jiwe moja moja.

Hata kwenye maisha yetu inabidi tuelewe kwamba, siku zote kuanza jambo lolote ni kitu kigumu sana. Mara nyingi inahitjika juhudi sana ili kuanza jambo, vinginevyo huwezi kuanza kabisa na pia najua unaelewa vizuri hili kuwa kuanza ni kugumu.

Kama wewe usipokuwa makini, utakuwa unatumia muda mwingi sana kufikiria kuhusu kuanza hasa ukifikiria ukubwa wa jambo unalotaka kulifanya na kujikuta unakata tamaaa au kuahirisha kwamba nitafanya siku nyingine.

Ni rahisi sana kupata msisimko na hamasa mara tu pale unapojiwekea malengo yako,  lakini kwa wengi linapokuja suala la kuchukua hatua hapo ndipo ugumu unapoanza na wengi husau kabisa kwamba siri ya mafanikio yao ipo kwenye kuanza.

Ili ufanikiwe unatakiwa uelewe hivi, chochote kitu kikubwa unachotaka kukitimiza, kinaanza na wewe kuchukua hatua ya kufanya au kinaanza na wewe kuchukua hatua  ya kuweka jiwe la kwanza ili kukamilisha  piramidi ya mafanikio yako.

Mwanzoni unapoanza kujenga mafanikio yako, unaweza ukaonekana si kitu wala huna chochote na hakuna unachofanya, lakini elewa huo ni mwanzo. Maajabu ya maisha yako ndipo yanapoanzia hapo kwa wewe kuamua kufanya.

Hutasogea na hautafanya mabadiliko yoyote ya maisha yako, ukiamua kutulia bila kufanya kitu. Fanikisha maisha yako na kuwa ya mafanikio kwa kuanza kitu kitakachokusogeza kwenye maisha yako.

Kila la kheri katika kufikia mafanikio  makubwa na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kwa ajili ya kujifunza na kuhamasika kila siku.

DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,

Ni wako rafiki katika mafanikio,

Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Blog, dirayamafanikio.blogspot.com
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com

No comments :

Post a Comment