Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Sunday, July 9, 2017

Jenga Nguvu Kubwa Ya Mafanikio Yako Kwa Kufanyia Kazi Mambo Haya Matatu.

No comments :
1. Kila wakati tafuta mafanikio yako kwa kufanya kile unachokipenda. Unapofanya kile unachokipenda utake usitake ni lazima utajituma tu bila hata kusukumwa. Kupenda kile unachokifanya, kazi kwako itakuwa ni kama mchezo na kwa kifupi ni rahisi tu kuwa mlevi wa kazi yaani ‘workaholic’ hasa kama unafanya kile unachokipenda.
Mara nyingi unapoona watu wanasukumwa sana katika kazi zao, na ni watu ambao kama hawajitumi ni rahisi kujua watu hao wanafanya kazi ambazo hawazipendi na wala hazipo kwenye mioyo yao. Wanafanya ili mradi siku ziende. Timiza mipango uliyojiwekea, kwa kuchagua kile unachokipenda kwenye maisha yako na kifanye.
2. Je, inafika wakati wakati katika maisha yako, wakati unang’ang’ana na kutimiza ndoto zako unajiona kama vile ndoto zako zinakuchanganya na kukukosesha raha?
Kama iko hivyo kwako, ni ishara tosha kabisa kwamba hutaki maisha yako yabaki hivyo, yaani kuna kitu ambacho unakitafuta na unataka kukibadili mara moja.
Mafanikio katika maisha hayaendi kwa watu walioridhika bali yanawafikia watu ambao kila wakijiangalia wanajiona hawana mafanikio kabisa.
3. Kipo kitu ambacho lazima unatakiwa kukifanya haijalishi una huzuni au unachangamoto nyingi sana, lakini unayo nafasi ya kufanya kitu ambacho kitaboresha maisha yako hata kama upo kwenye wakati mgumu sana.
Tuchulie huna pesa na limetokea tatizo kubwa, angalia kitu cha kufanya kitakachoweza kubadilisha hali yako hata kama ni kwa kidogo. Unapochukua hatua hiyo hata kama huwezi kubadili changamoto yako kabisa, lakini wewe utabadilika kwa sehemu.
Hivi ndivyo changamoto kubwa au matatizo makubwa yanatakiwa kukabiliwa. Haina maana kuiona nyumba yako ikiungua moto na kuiacha hivyo hivyo, kisa umeshindwa kuzima moto huo. Fanya kitu cha kukutoa katika hali ya yoyote uliyopo.
Kila la kheri katika kufikia mafanikio  makubwa uliyojiwekea.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Blog, dirayamafanikio.blogspot.com
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com

No comments :

Post a Comment