Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Monday, July 31, 2017

Nguvu Ya Kimafanikio Ipatikanayo Kwenye Uchaguzi Wako Sahihi.

No comments :
Safari ya kufikia mafanikio makubwa inaanza na kufanya uchaguzi uliobora. Hakuna mafanikio makubwa yoyote ambayo yanakuja kwa bahati mbaya, mafanikio yote makubwa yanaanza na uchaguzi uliobora na tena ambao unaufanya kila siku.
Uchaguzi huu ambao nina uzungumzia hapa na ukabadilisha maisha yako si uchaguzi mkubwa sana kama unavyofikiri. Huu ni uchaguzi mdogo mdogo ambao kuna wakati unayafanya hata pengine bila kufikiri.
Uchaguzi kama leo uamke saa ngapi, uchaguzi kama leo ujifunze nini au usijifunze, uchaguzi kama leo utumie pesa zako vipi, hizi ni moja ya chaguzi ndogo ndogo sana lakini ambazo ukizitumia vizuri zinabadilisha maisha yako kabisa na kuwa wa tofauti.

Ukumbuke kabisa kile unachokipata, ni matokeo ya kile unachokifanya, na kile unachokifanya ni matokeo ya uchaguzi unaoufanya kila wakati kwenye maisha yako. Kama unafanya uchaguzi mbovu, tegemea kupata maisha mabovu pia.
Matokeo bora kwenye maisha yako yanakuja kwa kufanya uchaguzi uliobora. Hiki ndicho kitu unachotakiwa ukielewe sana na kukifatilia. Ukijifunza kuwa na uchaguzi sahihi, itakusaidia sana kuweza kutimiza ndoto zako.
Acha kuendekeza uchaguzi mbovu utakaokangusha baadae. Acha kuendekeza kufanya uchaguzi wa kufanya starehe na kusahau kufanya kazi. Acha kuendekeza uchaguzi wa kuishi maisha uyatakayo badala ya kujenga nidhamu ya mafanikio.
Uchaguzi wowote unaoufanya ni lazima ulete matokeo. Kwa chochote kile unachotaka kukifanya wewe kifanye, ila hata hivyo uelewe majibu yake lazima utayapata, yawe mazuri au mabovu lakini uyapata bila shida.
Uchaguzi ule mdogo unaoufanya leo hata kama hautilii maanani, huo ndio unajenga msingi wa mafanikio yako ya kesho. Kuwa makini usije ukaishia kuishi maisha ya hovyo kama uchaguzi wako ni mbaya na haukusaidii.
Kumbuka, maisha yako yanaweza kubadilika ikiwa kama utafanya uchaguzi na maamuzi sahihi kila siku. Elewa hiyo ndiyo nguvu kubwa ya uchaguzi sahihi inavyofanya kazi na hata kukupa mafanikio utakayo.
Kila  la kheri katika kufikia mafanikio makubwa na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kujifunza kila siku.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Blog, dirayamafanikio.blogspot.com
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.comNo comments :

Post a Comment