google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Jul 1, 2017

KITABU; ANY THING YOU WANT(Kitu Chochote Unachokitaka).

No comments :
Uchambuzi wa kitabu katika aya moja.
Watu wengi katika maisha wanafanya mambo ambayo yanawapotezea furaha sana. Unapofanya biashara kumbuka kutengeneza sheria nzuri zitakazokusaidia kuongeza wateja wako. Pia Katika biashara usisahau jambo moja la msingi kwamba upo kwa ajili ya wateja wako.
Any Thing You Want (Kitu chochote unachokitaka).
Hata hivyo mwandishi wa kitabu hiki Derek Sivers, yapo mambo mengi ambayo ameyaongelea katika katika kitabu chake na yana manufaa kwako pia. Twende kwa pamoja tujifunze mambo mengine ya msingi yaliyoyachambuliwa, kwa kuangalia uchambuzi wa kitabu kizima.
1. Ipo tofauti kubwa kati ya kujiajiri kwenye biashara yako na kuwa mmiliki wa biashara yako. Unapokuwa umejiajiri katika biashara na ikatokea umetoka kidogo, kila kitu kitashindwa, lakini unapokuwa mmiliki wa biashara hata uiache biashara yako mwaka mzima, biashara hiyo itaendelea kuwepo.
2. Usifanye kitu chochote sababu kubwa ikawa  ni pesa, fanya mambo yako kwa ajili ya kutoa thamani, pesa itakuja yenyewe.
3. Hauwezi kujua sana vizuri kile kitu unachataka kukifanya, mpaka kitu hicho uanze kukifanya ndio utakijua kwa asilimia karibu zote.
4. Mafanikio yanakuja kwa kuendelea kuweka juhudi na kuboresha kila hali katika maisha yako. Endelea kuweka juhudi hata wakati mambo yanapokuwa hovyo.
5. Njia bora ya kukua kibiashara ni kwa wewe kuangalia kwanza wateja wako wa kwanza, kisha na kuendelea  kutafuta wateja wengine.
6. Ni muhimu kujua njia za kumlinda mteja wako kila wakati, ukiweza kufanya hivyo utajikuta upo vizuri kibiashara.
7. Jifunze mambo mwenyewe, kwa kujifunza mambo hayo itakusaidia sana kukua wewe na kukujengea mafanikio makubwa.
8. Kila wakati jenga tabia ya kuamini wengine unapokuwa kwenye biashara, lakini kuwa makini sana unapotaka kugawa majukumu yako.
9. Chochote unachokifanya, ujue huo ndio ubunifu wako. Fanya unachokifanya kwa ubora ili ndoto zako zitimie.
10. Unaweza ukawa na furaha sana hata kama una kiasi kidogo cha pesa, sio lazima una pesa nyingi sana ndio utengeneze furaha kubwa.
11. Kila wakati usisahau kwamba unaweza ukaweka sheria au kanuni za kukusaidia kupata chochote unachotaka na hilo linawezekana.
12. Weka mipango mingi ambayo unaona inaweza ikakusaidia kukufanikiwa. Hakuna njia moja ya mafanikio ambayo inasema hii ndio sahihi.
Chukua hatua na fanyia kazi mambo hayo muhimu uliyojifunza kutoka kwenye kitabu hiki na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Kama unamtaji mdogo, mtaji wa kati au mtaji mkubwa na unahitaji wazo bora la biashara litakalokutoa kimaisha, tafadhari usisite kuwasiliana nasi kwa 0713 048 035 au tutumie e-mail kwenda dirayamafanikio@gmail.com, kwa msaada zaidi.
Kila la kheri katika kufikia mafanikio makubwa,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Blog, dirayamafanikio.blogspot.com
Mawasiliano; +255 713 048 035,

Email; dirayamafanikio@gmail.com

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.