Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Tuesday, July 4, 2017

MAFANIKIO TALK: Mbinu Za Kupata Masoko Katika Biashara.

No comments :
Uhali gani mpenzi msomaji wa mtandao huu wa dira ya mafanikio, husasani kipindi hiki cha mafanikio talk kinachokujia kila siku ya jumanne, ambapo madhumuni ya kipindi hiki ni wewe kutushirikisha kile ulichonacho kinachohusu mafanikio.
Kinachofanyika hapa ni kwamba, mtandao huu wa DIRA YA MAFANIKIO unakupa fursa wewe mtanzania na usiye mtanzania kuweza kutushirikisha jambo moja lenye kuleta tija katika safari yetu ya mafanikio kwa namna moja ama nyingine.
Je, ungependa kushiriki katika kipindi hiki cha mafanikio talk  siku ya jumanne ijayo? Kama jibu ni ndiyo nakusihi usome mpaka mwisho wa makala haya, tutakueleza namna ya kushiriki na ukawa msaada kwa wengine.
Kwa hayo machache kati ya mengi kuhusu namna ya kushiriki kipindi hiki cha mfanikio talk nadhani inatosha, hivyo nikukaribishe kwa moyo mkunjufu katika kipindi chetu cha leo na siku ya leo tupo na mwanaharakati kutoka mkoa Tabora, anaitwa Justin Kasubi.
Tengeneza soko lako kwa uhakika.
Mwanaharakati huyu ni mpambanaji sana katika kufanya biashara tofauti tofauti pale mkoani Tabora, tulizungumza naye mambo mengi sana ya kimafanikio. Kati ya mambo hayo ni pamoja na kutushukuru sisi kwa elimu tunayoendelea kuitoa.
Hata hivyo pia ameshukuru kwa kwa elimu nyingine  ambayo hutolewa katika makundi yetu ya Whatsapp, anasema binafsi yamemsaidia sana kuweza kuimarika kifikra na kuweza kukua kibiashara kila kukicha.
Lakini licha ya kuzungumza mambo mengi na mwanaharakati huyu kubwa zaidi anasema anatamani sana kufahamu mambo mbalimbali yatakayomsaidia kuweza kutafuta masoko katika biashara yoyote ile.
Nasi kwa kuwa hatufungamani na upande wowote siku ya leo tutaeleza namna ya kutafuta masoko katika biashara kama ifuatayo;
Utafutaji wa masoko katika biashara yeyote ile ni muhimu sana, na tendo hili ni kila mmoja wetu ambaye anatamani kuingia katika ulimwengu wa biashara aweze kujua somo hili.
Kwanza kabisa utafutaji wa masoko ni hatua za awali ambapo mfanyabiashara ni lazima aweze kuelewa, kwani wengi wetu huingia katika biashara kisha wanaanza kutafuta wateja, kufanya hivi ni  sawa na kuvaa viatu kwanza, kisha soksi zinafuata.
Kwa muktadha huo ni kujichelewesha mwenyewe katika safari yako ya mafanikio, hivyo mbinu bora ya kutafuta masoko ni heri kufikiri kwa umakini mwanzoni kabisa  kabla ya kuanza kufanya biashara fulani.
Unatakiwa ujenge tabia ya kujiuliza kwamba katika kitu hiki ninachotaka kufanya hivi wateja wangu watakuwa ni wakina nani? Na wanapatikana wapi? Unatakiwa upate majibu halisi ya haya maswali ili ujue ni kipi cha kufanya.
Mara baada ya kupata majibu ya maswali hayo?  Nenda mahali husika na kutazama wafanyabiashara wengine wenye biashara kama ya kwako, na kuangalia  wao wanatumia mbinu zipi kupata wateja wengi?
Mara baada ya kupata majibu hayo, zama katika halmashauri ya ubongo wako na ufikiri kwa kina namna ambavyo utaweza kuwa mbunifu kuwashinda washindani hao. Tafuata majibu pia ni ubunifu upi utakaouweka.
Lakini mwisho kabisa mbinu bora ya kutafuta masoko ni kutangaza biashara yako, asikwambie mtu biashara ni matangazo. Unaweza kutangaza biashara kupitia vyombo vya habari, mitandao ya kijamii na sehemu zinginezo.
Hivyo kwa mbinu yeyote ambayo utaamua kuitumia ni vyema ukahakikisha inaleta wateja wapya, na wateja hao hakikisha pia huwapotezi. Ikiwa unawapoteza wateja wako, basi utakuwa hufanyi kitu, unakuwa kama unacheza.
Mpaka hapo hatuna la ziada siku ya leo tukutane jumanne ijayo katika kipindi hiki cha mafanikio talk. Kama unatamani siku ya jumanne ijayo tuweze kutupa somo kutoka kwako tuma neno mafaniko talk kwenda 0757909942 au tuma neno hilohilo kwenda e-mail yetu dirayamafaniko@gmail.com nasi tutakutafuta kwa ajili ya mahojiano mubashara.
Asante sana kwa kuwa nasi  nikutakie siku njema na mafanikio mema. Endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza na kupata mwangaza halisi wa maisha yako.
Ni wako afisa mipango Benson Chonya,


No comments :

Post a Comment