google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Feb 9, 2018

Chanzo Cha Kutoelewana Kwingi Kinasababishwa Na Jambo Hili.

No comments :

Upo muda iwe kazini au katika maisha yetu ya kawaida, kunakuwa na kutokuelewana sana kati yako wewe na wale wanaokuzunguka. Kwa mfano, unakuta maelewano yanakuwa sio mazuri sana na kunakuwa na kupishana kwingi.
Umeshawahi kujiuliza nini huwa chanzo cha kutokuelewana vizuri, iwe kwenye familia, kazini au eneo lingine la maisha yetu hali ambayo husababisha migogoro sana. Kwa jinsi ilivyo chanzo kingi cha kutoelewana husababishwa na jambo moja tu, ambalo ni kutokuwaelewa wengine vizuri.

Moja ya kitu cha muhimu sana ambacho unatakiwa kuwa nacho kwenye maisha yako ni kuwa na uwezo wa kuwaelewa watu wengine pia ili kuepusha migogoro isiyo ya lazima. Hiyo yote ni kwa sababu tumeumbwa watu tukiwa wa tofauti, hivyo ni lazima uwaelewe watu wengine.

Ni muhimu kujua wewe ni wa tofauti huwezi kufanana na mwingine kwa mambo mengi. Kwa hiyo swala la kuendana na watu wengine jinsi walivyo hutakiwi kupuuza hata kidogo ndio maana tunasema ni muhimu sana kuwaelewa wengine vizuri.
Unapowaelewa watu wengine vizuri kabla hujaanza nao kufanya kazi yoyote, inakusaidia sana kukuondolewa wewe msongo wa mawazo na inaondoa kwako migongano ambayo ungekutana nayo bila sababu yoyote.
Jaribu kujiuliza ni mara ngapi umepatwa na hasira kwasababu ya jambo ambalo umekuja kugundua kwamba alaa kumbe ilikuwa ni kitu tu cha kutokuelewana. Unapokuja kugundua hivyo unakuwa tayari umepoteza nguvu na muda wako sana.
Inahitaji utulivu kidogo ili kuweza kuwaelewa wengine wanataka nini na wewe unataka nini ili mweze kwenda pamoja. Ikiwa itakuwa kinyume ya hapo utaanzisha mgogoro ambao hukutakiwa kuanzisha, lakini kisa ni maelewano mabovu.
Unatakiwa kujua ni rahisi tu kugombana na kila mtu ikiwa huwezi kuwaelewa watu vizuri. Uwe na uhakika utagombana na familia yako, utagombana na wenzako kazini na marafiki zako kwa sababu ya kushindwa kuleta maelewanao kati yenu ambayo yalikuwa ni rahisi kueleweka.
Kila siku ipo nafasi ya wewe kuweza kujenga uelewa wako kwa wanao kuzunguka. Unakuwa na nafasi ya kujenga maelewano na watu wanaokuzunguka hiyo ni faida kubwa sana kwako ya kudumisha mahusiano.
Unapokuwa unaelewa kujenga mahusiano mazuri, elewa haufaidiki wewe tu, hata wanao kuzunguka nao wananaanza kufaidika kwa kulewana kwa ufasaha ambako inakuwa tayari wewe kumekujenga na kukudumisha.
Kuanzia leo usikubali uwe chanzo cha mgogoro kwa sababu tu ya kutoelewana. Jenga maelewano mazuri sana karibu katika kila eneo na hiyo itakusadia sana kuweza kuweza kujenga mahusino mazuri na yatakayokupa pia mafaniko kwenye maisha yako.

Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatumia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Pia kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,






No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.